MAPYA YAIBUKA KIFO CHA PAPA WEMBA, YADAIWA ALIWEKEWA SUMU KWENYE MIC PHONE
Na MITANDAO
MAPYA yameibuka kufuatia kifo cha mwanamuziki gwiji barani Afrika Papa Wemba raia wa DRC aliyeanguka jukwaani na kufariki dunia huko Abidjan Ivory Coast imefahamika kuwa mwanamuziki huyo aliuawa kwa kuwekewa sumu.
Kwa mujibu wa taarifa moja iliyoenea mitandaoni ikionyesha video ya msanii huyo akiwa jukwaani alibadilishiwa Microphone nyingine ambayo ina sumu, kwani mkongwe huyo hakuweza kudumu nayo na alianguka ghafla ya kupoteza maisha.
Ripoti hiyo si nzuri sana kwani inasema kuzusha uhasama mwingine ambao unaweza kulipeleka mahakamani, Papa Wemba muasisi wa muziki wa kizazi kipya wa Soukous alifariki dunia Aprili 14 Abidjan baada ya kuanguka jukwaani akitumbuiza.
Mwili wake uliwasili DRC juzi na anatarajia kuzikwa Jumanne ijayo, marehemu Papa Wemba atakumbukwa kwa nyimbo zake nzuri ikiwemo Shomy the Way