AZAM FC YAISHUSHA SIMBA, YAICHAPA MAJIMAJI 2-0
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM
AZAM FC jioni ya leo katika uwanja wake wa Azam Complex Chamazi imewafumua Wandengeleko kutoka Ruvuma Majimaji mabao 2-0 mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Shujaa wa Azam katika mchezo huo alikuwa Mudathili Yahya aliyefunga magoli yote mawili, kwa matokeo hayo Azam imechupa hadi nafasi ya pili ikiiondoa Simba ambayo sasa imeangukia nafasi ya tatu.
Majimaji licha ya kucheza kandanda zuri na la kuvutia lakini ilijikuta ikinyukwa mabao hayo yaliyoifanya Azam ifikishe pointi 58 na mechi 25 ikiwa nyuma ya mabingwa watetezi Yanga wenye pointi 62 baada ya leo hii kuichapa Mgambo JKT mabao 2-1.
Jumapili ijayo uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Azam Fc itakutana na Wekundu wa Msimbazi Simba Sc mchezo wa ligi kuu bara ambao utaamua nani ataingia kwenye vita ya kuwania ubingwa wa bara