HATIMAYE MWANZA WAPATA TIMJ YA PILI LIGI KUU

Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM

SHIRIKISHO la kandanda nchini TFF limeipandisha ligi kuu timu ya Mbao Fc ya Mwanza na kuufanya mkoa huo kuwa na timu mbili zitakazoshiriki ligi kuu bara kwa pamoja na kuwa historia.

Mkoa wa Mwanza haukuwahi kuwa na timu mbili kwa pamoja kwa muda mrefu tangia Pamba Fc pia ya Mwanza iliposhuka daraja na kuiacha Toto Africans ikiendelea kutesa hadi sasa.

TFF imeamua kuipandisha Mbao Fc ligi kuu kufuatia kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo kuzishusha daraja timu nne kwa mkupuo za Geita Gold, Polisi Tabora, JKT Kanembwa na JKT Oljoro kwa kupanga matokeo.

Geita Gold iliifunga mabao 8-0 timu ya JKT Kanembwa ya Kigoma na Polisi Tabora nayo ikaichapa mabao 7-0 timu ya JKT Oljoro ya Arusha na baadaye kuibuka mgogoro mkubwa kuwa timu hizo zimepanga matokeo ambapo TFF ikaamua kuzishusha daraja na baadhi ya wachezaji, viongozi na marefa wakafungiwa miaka kumi hadi maisha.

Mbao Fc ilikamata nafasi ya nne kwenye kundi lake la C lililojumuhisha timu hizo zilizoshushwa daraja, hivyo wanabahatika kuokota dodo kwenye mfenesi, msimu ujao watashiriki ligi kuu bara na kufanya sasa kanda ya ziwa kuwa na timu tano ambazo ni Toto Africans na Mbao Fc za Mwanza, Stand United na Mwadui Fc za Shinyanga na Kagera Sugar ya mkoani Kagera

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA