FARID MUSSA KIMEELEWEKA HISPANIA, BAKHRESSA AMPANDIA NDEGE KUMALIZANA NAO
Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM
WINGA kinda wa klabu bingwa Afrika mashariki na kati Azam Sc, Farid Mussa Mariki anaelekea pazuri katika majaribio yake na huenda akafuzu hasa baada ya kuwashangaza kwenye mchezo wa kirafiki kati ya CD Tanarife timu anayoichezea kwa sasa na UD Diabora.
Kinda huyo atakayefanya majaribio ya mwezi mmoja na timu hiyo ameonyesha kiwango kizuri na tayari uongozi wa timu hiyo umeshaanza kuwasiliana na mabosi wa Azam ambapo Yussuf Bakhressa ameshapanda pipa kufuatilia dili.
Farid atakuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kucheza soka la kulipwa miaka hii sasa mara baada ya kuanzishwa soka la kulipwa, winga huyo ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars amekuwa msaada kwenye klabu yake ya Azam kwani ndiye muuaji wa bao dhidi ya Esperance ya Tunisia, Azam ikishinda 2-1 uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es Salaam