SIMBA KUMREJESHA OKWI, KUACHANA NA KIIZA

Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM

IMEBAINIKA klabu ya Simba ipo katika mipango ya mwisho ya kumrejesha mshambuliaji wake wa zamani Mganda Emmanuel Okwi na pia ikitaraji kuachana na Mganda mwenzake Hamisi Kiiza 'Diego'.

Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho kipo karibu na klabu hiyo kimesema tayari viongozi wa timu hiyi wameshakubaliana kumrejesha nyota huyo kipenzi cha mashabiki wa Simba.

Okwi aliuzwa na Simba mwishoni mwa msimu uliopita kwa klabu ya Sonderjyske ya Denmark inayoshiriki ligi kuu lakini maendeleo yake si mazuri ndani ya timu hiyo na imetangaza kumpiga bei.

Uongozi wa timu hiyo umewasiliana na Simba na kukubalina kwamba Okwi atauzwa kwa hela ileile iliyotumika kumnunua, kwa maana hiyo Simba sasa itafufua matumaini yake ya kufanya vizuri msimu ujao kwani mshambuliaji huyo ana msaada mkubwa ndani ya klabu hiyo.

Wakati Okwi anarejea Simba, mshambuliaji Hamisi Kiiza huenda akatupiwa virago, Kiiza aliyebakisha miezi michache kumaliza mkataba, anapigiwa hesabu za kuachwa kutokana na maelewano yake kuwa madogo na kocha wake Jackson Mayanja raia wa Uganda

Emmanuel Okwi raia wa Uganda, anarudi Simba

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI