JUMA ABDUL AISOGEZA YANGA KARIBU NA UBINGWA
Na Ikram Khamees, MWANZA
BAO lililofungwa na beki wa kulia Juma Abdul Mnyamani limetosha kabisa kuisogeza Yanga Sc jirani na ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya jioni ya leo kuichapa Toto Africans mabao 2-1 uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Wakicheza vizuri kabisa chini ya kocha wao John Tegete, Toto Africans walionekana kuidhibiti Yanga idara zote na dakika ya 39 kipindi cha kwanza walijipatia bao la kuongoza lililofungwa na William Kimanzi.
Hadi mapumziko Toto walikuwa mbele kwa bao hilo moja, kipindi cha pili Yanga walirejea kwa kasi ya aina yake na dakika ya 8 Amissi Tambwe aliisawazishia timu yake, Yanga waliongeza bao la pili lililofungwa na Juma Abdul Mnyamani kufuatia makosa ya mabeki wa Toto.
Kwa ushindi huo wa leo, Yanga sasa imefikisha pointi 65 na mechi 26 hivyo ikizidi kupaa kileleni, mechi nyingine tatu zimechezwa leo ambapo mjini Shinyanga Mwadui imewaalika majirani zao Stand United, Prisons wameialika JKT Ruvu na jijini Tanga Africans Sports wamekipiga na Coastal Union uwanja wa Mkwakwani, kesho uwanja wa Taifa Dar es Salaam Simba Sc watakutana na Azam Fc