AZAM FC YAIPASHIA MISULI SIMBA, NGOMA KUPIGWA JUMAPILI, SIMBA WATUA JANA KIMYAKIMYA

Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM

WAKATI klabu ya Simba ikiwasili Dar es Salaam jana kimya kimya, wapinzani wao Azam Fc wao wameendelea na mazoezi yao kabambe katika uwanja wao wa Azam Complex Chamazi.

Azam Fc inacheza na Simba Sc mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara uwanja wa Taifa Dar ea salaam, Simba wao walienda Zanzibar kuweka kambi kujiandaa na mchezo huo na juzi usiku waliichapa Mafunzo mabao 3-0 yaliyofungwa na Awadh Juma kama sehemu ya kujiandaa na mchezo huo.

Hadi sasa Azam Fc inashika nafasi ya pili wakiwa nyuma ya vinara Yanga Sc na wana pointi 58 na mechi 25 sawa na Simba anbayo yenyewe inashika nafasi ya tatu na pointi 57, Yanga iko kileleni ikiwa na pointi 62 na mechi 25.

Mchezo wa Azam na Simba utakuwa mgumu kwakuwa kila timu inataka kuibuka na ushindi ili kulisogelea taji la ubingwa wa bara ambalo linashikiliwa na Yanga, Simba inanolewa na Jackson Mayanja raia wa Uganda wakati Azam yenyewe inanolewa na Stewart Hall raia wa Uingereza, Nani ataibuka

Wachezaji wa Azam wakiwa mazoezini
Kocha Stewart Hall akiwaelekeza wachezaji wake jinsi ya kuwaua Simba Jumapili

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA