YANGA WATANGULIA FAINALI FA CUP, MAWE YAVULUMISHWA MKWAKWANI

Na Mkola Man, TANGA

MABINGWA wa soka Tanzania bara Yanga Sc jioni ya leo imefanikiwa kuchomoza na ushindi katika uwanja wa Mkwakwani Tanga baada ya kuilaza Coastal Union mabao 2-1 mchezo wa Nusu fainali kombe la FA.

Licha kwamba mchezo huo haukumalizika kutokana na muda wake hasa mashabiki wa Coastal Union kuwapiga mawe wachezaji wa Yanga wakianza na kipa wake Deogratus Munishi 'Dida'.

Mchezo huo ilibidi uende kwenye muda wa nyongeza yaani dakika 30 baada ya kumaliza dakika 90 wakifungana 1-1, Coastal walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Yousef Sabo raia wa Cameroon.

Goli hilo lilipatikana kipindi cha pili baada ya kumaliza dakika 45 za kwanza 0-0. Yanga nao wakacharuka na kufanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa Donald Ngoma raia wa Zimbabwe.

Yanga tena walipata bao la pili katika muda wa nyongeza kupitia kwa Amissi Tambwe raia wa Burundi aliyepokea krosi ya Juma Abdul Mnyamani.

Kwa maana hiyo Yanga wanaingia fainali na sasa watakutana na Azam Fc ambayo iliwagaragaza Mwadui Fc mabao 2-1 uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga

Yanga wakishangilia 

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA