AZAM FC YATINGA FAINALI YA FA CUP, YAWACHAPA MWADUI KWA PENALLTI 5-3

Na Paskal Beatus, SHINYANGA

AZAM FC jioni ya leo imetinga fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup baada ya kuilaza Mwadui Fc kwa mikwaju ya penalti 5-3 baada ya kumaliza dakika 90 zikiwa sare ya 2-2 uwanja wa Mwadui Complex mchezo wa Nusu fainali.

Kwa matokeo hayo Azam Fc imeingia fainali na sasa inaweza kukutana na Yanga ambayo ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union uwanja wa Mkwakwani Nusu fainali nyingine, mchezo huo ulivunjika zikiwa zimebaki dakika 10.

Azam walipata magoli ya Azam yaliwekwa kimiani na Hamisi Mcha "Vialii" wakati yale ya Mwadui yalifungwa na Jabir Aziz "Stima" na Kevin Sabato.

Timu hizo zilienda kwenye mikwaju ya penalti baada ya muda wa nyongeza dakika 30 kukamilika, Azam walipata penalti zao kupitia kwa John Bocco "Adebayor", Waziri Salum, Himid Mao Mkami, Allan Wanga na Agrey Morris aliyefunga ya ushindi.

Mwadui nao walipata penalti zao tatu kupitia kwa Malika Ndeule, Iddi Mobby na Jabir Aziz wakati Kevin Sabato alikosa

Azam Fc wametinga fainali ya FA Cup

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA