YANGA WATUA DAR NA KUFIKIA TIFFANY HOTEL KUWANGOJA MGAMBO JKT
Na Ikram Khamees, DAR EA SALAAM
YANGA SC imewasili Dar es Sala leo ikitokea mkoani Tanga ambako jana iliwalaza Coastal Union ya Tanga mabao 2-1 mchezo wa Nusu fainali michuano ya FA Cup na kutinga fainali.
Mabingwa hao wa bara Jumatano ya keshokutwa wanashuka uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuwakaribisha Mgambo JKT mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Yanga ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 59 wakicheza mechi 24 wakifuatiwa na Simba wenye pointi 57 wenye mechi 25, endapo Yanga itashinda mchezo huo itazidi kujikita kileleni