MPYA KUHUSU COASTAL UNION, YADAIWA AZAM INATIA MKONO KUIUA, KISA BIASHARA
Na Mkola Man, TANGA
MPYA nadhani hakuna yeyote anayefahamu taarifa hiyo ni kwamba klabu ya Coastal Union ya Tanga inahujumiwa na Azam ambao ndio wadhamini wa mashindano ya Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup.
Habari za uhakika ambazo Mambo Uwanjani imezinyaka kuwa hata katika mchezo wa jana kati ya Yanga na Coastal Union uwanja wa Mkwakwani Tanga, Azam imehusika kwa namna moja ama nyingine ingawa ni ngumu kuamini.
Ishu iko hivi, mdhamini mkuu wa Azam Fc ni kampuni ya Azam Food Production watengenezaji wa bdhaa mbalimbali ukiwemo unga wa ngano na sembe, wakati mdhamini mkuu wa Coastal Union ni kampuni ya Pembe watengenezaji wa unga bora wa ngano na sembe.
Ushindani wa makampuni unaweza kuwa mkubwa endapo tu Coastal itapata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa, kwa sasa Coastal imepote,a mwelekeo kwenye ligi hivyo nafasi walikuwa nayo kupitia FA Cup.
Inadaiwa Azam imetia mkono ili Coastal isipate nafasi ya kuonekana kimataifa kwani itaathili biashara ya Azam, lakini kikosi cha Coastal kipo vizuri sana huwezi kuamini