YANGA YAFA KISHUJAA LIGI YA MABINGWA AFRIKA, YAPIGWA 2-1 YAANGUKIA SHIRIKISHO
Na Exipedito Mataruma, ALEXANDRIA
MABINGWA wa Tanzania bara Yanga Sc wameondoshwa katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika bada ya kufungwa kishujaa mabao 2-1 na Al Ahly ya Misri mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa Borg Al Arab mjini Alexandria usiku ya Jumatano.
Katika mchezo huo Yanga ilixheza vizuri muda wote na kulisakama lango la Al Ahly kiasi kwamba mwamuzi wa mchezo huo alipopuliza kipyenga kuashiria mpira umemalizika mashabiki wa Al Ahly walishangilia kama wametwaa ubingwa wa Afrika.
Kwa sasa unaweza kutamka kuwa Yanga na Al Ahly ni kama wapinzani wa jadi katika soka la Afrika kutokana na ushindani ulioonyeshwa usiku huu, Al Ahly walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Hossam Ghaly.
Bao lilipatikana kipindi cha pili dakika ya 52 baada ya kuunganisha kwa kichwa kona ya Ahmed Fathi, Yanga walitulia na kucheza soka la kitabuni na kufanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia mshambuliaji wake Mzimbabwr Donald Ngoma kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Juma Abdul.
Goli hilo la kusawazisha lilipatikana dakika ya 57, wakati wengi wakiamini mchezo huo unaweza kumalizika kwa sare ya 1-1 hasa baada ya kwisha kwa dakika 90 za kawaida mwamuzi aliongeza dakika 5, hapo ndipo yalipotokea maajabu ya soka kwani Abdallah Saed aliukwamisha mpira kimiani na kuwaondosha Yanga mashindanoni.
Yanga sasa itaangukia kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo ratiba yake inatarajia kupangwa Alhamisi, na huenda ikakutana na Esperance ya Tunisia katika mchezo ujao