MICHANO: HUSSEIN MACHOZI, BAADA YA KUVIMBA KICHWA, AKAKIMBILIA KENYA AKAWASAHAU MASHABIKI WAKE BONGO
Na Mkola Man, TANGA
YAP....Yap...yap...Michano yangu ya leo inamchana Mmasai wa Singida ajulikanaye kwa jina la Hussein Machozi mkali wa bongofleva aliyeiibukia jijini Mwanza chinj ya meneja wake Kid Bway.
Mbali na muziki pia ni mwanasoka mzuri na kwa mara ya kwanza nilikutana naye Tanga katika studio za Motika Record chini ya marehemu Mr Ebbo.
Mimi nilienda kurekodi wimbo wangu uitwao "Utajiri hewa",niliomshirikisha Mr Ebbo kwenye kiitikio, toka hapo hatujaonana tena ila kwa sasa yupo nchini Kenya.
Alifahamika sana kwa nyimbo zake za mikasa kama vile 'Kafia gheto', 'Jela' na nyimbo nyinginezo ambazo zilimfanya avimbe kichwa hadi kupasuka.
Kupotea kwenye gemu ya muziki kwa Hussein Machozi ni kutokana na kuachana na meneja wake akiamini atajiendesha mwenyewe akisahau kuwa thamani ya kidole ni pale kinapoondoka, kiufupi kwa sasa kaishiwa pumzi.
Jamaa ilifikia hatua hadi anataka kurudia tena kucheza soka, akaenda kufanya mazoezi Kagera Sugar timu aliyowahi kuitumikia hukp nyuma, yaani Machozi anatokwa machozi kwani huko Kenya kaenda bila mashabiki wake.
Yap Mkola Man naendelea kuwepo inshallah tumuombe mungu tukutane wiki ijayo.
Mwandishi wa kolamu hii ni msanii wa Hip Hop maskani yake Tanga