TCHETCHE FITI KUIVAA SIMBA J,PILI

Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa klabu bingwa Afrika mashariki na kati Azam Fc Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast huenda akawepo katika kikosi cha timu hiyo kitakachoivaa Simba Sc uwanja wa Taifa Dar ea Salaam.

Tchetche alikosa mechi kadhaa za mashndano matatu tofauti akisumbuliwa na misuli, Simba na Azam zinakutana Jumapili ya keshokutwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Mshambuliaji tegemeo alikosa mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Esperance ya Tunisia ambapo Azam iliondolewa kwa jumla ya mabao 4-2.

Aidha mshambuliaji huyo alikosa mchezo wa Nusu fainali kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup dhidi ya Nwadui Fc ya Shinyanga ambapo Azam ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-3.

Pia aliukosa mchezo wa ligi kuu bara dhidi ya Majimaji ambao Azam ilishinda 2-0, kurejea kwa mshambuliaji huyo kunaongeza joto la mchezo huo

Kipre Tchetche fiti kuivaa Simba

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA