YANGA YAKARIBIA KUMREJESHA HAMISI KIIZA
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TAYARI jina la mshambuliaji wa Simba Hamisi Kiiza "Diego" limeshafika mikononi mwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga bilionea Yusuf Manji na muda wowote wanaweza kumasajili.
Mahambuliaji huyo raia wa Uganda anaelekea kumaliza mkataba wake na amekuwa haelewani na kocha wake Mganda mwenzake Jackson Mayanja.
Yanga wanataka kumpa kazi moja ya kusaidiana na Mzimbabwe Donald Ndombo Ngoma baada ya Mrundi Amissi Tambwe kuonekana kushuka kiwango katika siku za hivi karibuni.
Lakini mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Sc Zacharia Hanspoppe yeye amesema Kiiza ni mali yao na hawana mpango wa kumwachia kwa sasa, Hanspoppe amedai mchezaji huyo ataendelea kukipiga Msimbazi hadi msimu utakapomalizika na wamepanga kumuongeza mkataba mwingine