BAADA YA KUTUA KUTOKA TUNISIA, AZAM WAIFUATA MWADUI

Na Exipedito Mataruma, DAR ES SALAAM

KLABU bingwa Afrika mashariki na kati Azam Fc wamewasili leo na moja kwa moja kuunganisha ndege kuelekea Mwanza tayari kabisa kuwavaa Mwadui ya Shinyanga mchezo wa FA Cup Jumapili ijayo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam, mtendaji mkuu wa Azam, Saad Kawemba amedai vijana wake wako sawasawa kushinda.

Bingwa wa michuano ya kombe la FA anapata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, Azam imewasili leo kutoka Tunis, Tunisia ilikokwenda kurudiana na Esperance ambapo iliondoshwa kwa jumla ya mabao 4-2, Katika mchezo huo Azam ililala 3-0 na mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam, Azam ilishinda 2-1

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA