YANGA KUANGUKIA MIKONONI KWA WAARABU
Na Prince Hoza, DAR E SALAAM
YANGA SC ya Tanzania inaweza kuangukia tena mikononi mwa timu za waarabu endapo Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF litaamua kufanya hivyo leo.
Yanga ambayo jana usiku iliondolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kufungwa mabao 2-1 na Al Ahly ya Misri katika uwanja wa Borg Al Arab mjini Alexandria.
Jumla Yanga imefungwa mabao 3-2, na kutolewa kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika, kwa maana hiyo Yanga imeangukia kombe la Shirikisho barani Afrika na inaweza kukutana tena na timu za uarabuni.
Timu ambazo zinaweza kukutana na Yanga ni Kawkab Marakech ya Morocco, Mounana ya Gabon, Misr Makkassa ya Misri, Medeanna ya Ghana, FAR Rabbat ya Morocco, Esperance ya Tunisia, Sagrade Esperance ya Angola au Stade Gabesien ya Tunisia.
Yanga vilevile inaweza kuangukia mikononi mwa timu za ES Sahel ya Tunisia, Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini, Al Ahly Benghazi ya Libya, TP Mazembe ya DRC, El Merreikhy ya Sudan, MO Bejala ya Algeria ama Stade Mallen ya Mali