STAA WETU: HASSAN KABUNDA, MTOTO WA NINJA WA YANGA ANAYEING' ARISHA MWADUI FC
Na Paskal Beatus, SHINYANGA
JINA la Hassan Kabunda linaonekana kama geni masikioni mwa watu, lakini wapo wanaomkunbuka beki wa zamani wa Tukuyu Stars, Yanga Sc na timu ya taifa ya Tanzania bara Kakakuona Salum Kabunda 'Ninja' ukipenda Msudan.
Beki huyo alijulikana kwa kucheza kibabe sana uwanjani mpaka ikafikia washambuliaji kuanza kumuogopa, Hassan Kabunda ni mtoto wa Salum Kabunda, lakini iko tofauti kidogo.
Hassan Kabunda yeye ni mshambuliaji na si beki kama ilivyokuwa kwa baba yake, kijana huyu amekuwa katika kiwango kizuri na kuwa msaada mkubwa kwenye timu yake ya Mwadui Fc ya Shinyanga.
Kabunda ni mshambuliaji wa timu hiyo na anakumbukwa vizuri hasa pale alipoifungia Mwadui mabao yote mawili dhidi ya Coastal Union mchezo wa ligi kuu bara Nwadui ikishinda ikishinda mabao 2-1.
Nyota huyo aliibukia katika mashindano ya Copa Cocacola akiwa na timu ya Mkoa wa Ilala, Kabunda akiwa na ndugu yake Ally Kabunda wote washambuliaji, walitamba katika michuano hiyo na baadaye wakasajiliwa na Ashanti inayoshiriki ligi Daraja la kwanza.
Kabunda amekuwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza mashambulizi na anapokosekana uwanjani pengo lake linaonekana dhahili, mshambuliaji huyo anaichezea Mwadui Fc ya mjini hapa anbayo inanolewa na Jamhuri Kihwelu 'Julio'.
Umuhimu wake ulionekana katika mchezo wao wa ligi kuu bara dhidi ya mabingwa watetezi Yanga Sc uliopigwa uwanja wa Taifa Dar esvSalaam ambapo Yanga ilishinda 2-1, baada ya Mwadui kumtoa Kabunda na kumwingiza mkongwe Nizar Khalfan Yanga walionekana kupata ahueni kidogo.
Alipokuwepo uwanjani Kabunda, Yanga walishindwa kulifikia lango la Mwadui na matokeo yalikuwa 1-1 kipindi cha pili, lakini mabadiliko aliyoyafanya Julio ya kumtoa Kabunda yakawafanya Yanga wapande mbele na dakika ya 87 Haruna Niyonzima akaifungia Yanga bao la pili.
Kama mwalimu wa timu ya taifa, Taifa Stars Charles Boniface Mkwassa yatamulika vizuri basi kijana huyo anaweza kuwemo kwenye kikosi chake kwani ni miongoni mwa wachezaji wanaofaa kuitumikia