HANSPOPPE AMRUKA BASENA, ASEMA SIMBA HAWANA MPANGO NAYE
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM
BAADA ya kuripotiwa kwenye vyombo vya habari kwamba kocha wa zamani wa Simba Moses Bassena raia wa Uganda anawasili nchini tayari kabisa kwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Simba.
Lakini mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Wekundu hao wa Msimbazi Kapteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Zacharia Hanspoppe amesema hawana mpango wa kumuajili kama kocha mkuu wa Simba Mganda huyo.
Hanspoppe amekiri ni kweli Simba iko mbioni kutafuta kocha mpya atakayeiongoza timu hiyo msimu ujao lakini si Bassena, amedai uwezo wa Bassena hautofautiani na ule wa Jackson Mayanja hivyo wao wanasaka kocha wa matawi ya juu.
Mayanja alichukua jukumu la kuiongoza Simba kama kocha wa muda baada ya Muingereza Dylan Kerr kutupiwa virago, Simba kwa sasa inakamata nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 nyuma ya Yanga yenye pointi 59 ila imecheza mechi 26 wakati Yanga imecheza mechi 25