KASEKE AING' ARISHA YANGA KILELENI
Na Saida Salum, DAR ES SALAAM
DEUS Kaseke ameifungia Yanga mabao mawili muhimu jioni ya leo uwanja wa Taifa Dar es Salaam ikiifunga Mgambo JKT ya Tanga mabao 2-1 mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Mgambo JKT ilitangulia kupata bao la kuongoza dakika ya nne likifungwa na Nassoro Gumbo, Yanga walipambana kuhakikisha wanasawazisha bao na walifanikiwa kusawazisha lililofungwa na Deus Kaseke.
Hadi mapumziko timu hizo zilienda sare ya 1-1, kipindi cha pili kilianza kwa kasi nyingine huku Yanga ikijaribu kuwaingiza nyota wake wanaotamba kama Donald Ngoma na Thabani Kamusoko.
Yanga waliongeza bao la pili lililofungwa na yule yule Deus Kaseke, hadi mpira unakwisha matokeo ndio hayo, Yanga sasa imefikisha pointi 62 na mechi 25 ikiendelea kung' ara kileleni