KIZUGUTO NJE, ALFRED LUCAS AFISA HABARI MPYA TFF
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limemteua Alfred Lucas kuwa Afisa Habari na Mawasiliano mpya wa shirikisho hilo kuanzia leo Aprili 27, 2016.
Lucas mwandishi wa habari wa siku nyingi nchini wa magazeti mbalimbali likiwemo la Dimba anachukua nafasi ya ndugu Baraka Kizuguto aliyehamishiwa ofisi nyingine.
Kizuguto anakwenda kuwa Afisa mashindano na meneja mifumo Pepe ya usajili kwa TMS, Alfred ana uzoefu kutoka kwenye vyombo vya habari mbalimbali alivyovitumikia kama mwandishi wa habari na mhariri likiwemo gazeti la Dimba ambalo lilimuinua kabla hajaenda magazeti mengine.
Kadhalika Alfred kitaaluma amesomea uandishi wa habari na uhusiano wa kimataifa na diplomasia pamoja na lugha