YANGA NAO WAWASILI TOKA MISRI NA KUELEKEA TANGA
Na Exipedito Mataruma, DAR ES SALAAM.
Mabingwa wa Tanzania bara Yanga Sc wamewasili leo kutokea nchini Misri ambako waliondoshwa katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika na Al Ahly kwa jumla ya mabao 3-2.
Yanga ilitua leo na moja kwa moja kuanza safari ya kuelekea jijini Tanga ambapo Jumapili ijayo itaumana na Coastal Union mchezo wa Nusu fainali kombe la FA.
Kikosi cha Yanga kilichopata mapokezi makubwa uwanja wa Mwl Nyerere kinapewa nafasi kubwa kulipiza kisasi katika mchezo huo kwani zilipokutana ligi kuu bara Yanga ilichapwa 2-0.
Coastal wameonekana kubadilika katika siku za karibuni na hawatakubali kirahisi kupoteza mchezo huo na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika