YANGA WAFANYA MAZOEZI MAKALI MCHANA NA USIKU, TAYARI KABISA KUWAMALIZA WAARABU KESHO

Na Exipedito Mataruma, MISRI

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika Yanga Sc, wanaendelea kujifua vikali katika uwanja wataochezea mechi yao ya marudiano na Al Ahly ya hapa Misri kesho.

Kocha wa Yanga Mholanzi Hans Van der Pluijm ameiambia Mambo Uwanjani kwamba vijana wake wanafanya mazoezi makali ya kuwamaliza kabisa Waarabu hiyo kesho.

Yanga inahitaji sare ya mabao zaidi ya moja ama mawili ili iweze kusonga mbele lakini amedai hawezi kupoteza mchezo huo.

Timu hizo zinarudiana kesho baada ya mchezo wa kwanza kutoka sare ya 1-1 jijini Dar es Salaam, Al Ahly itakuwa na kazi nyepesi kwani tayari ina bao la ugenini ililolipata Dar es Salaam.

Endapo itatokea Yanga kushinda mchezo huo itakuwa imeingia hatua ya makundi, na kama bahati mbaya imetolewa itaangukia kombe la shirikisho barani Afrika

Yanga wakiwa mazoezini

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA