ANAYEKUMBUKWA LEO: SAIDI MWAMBA "KIZOTA". MSHAMBULIAJI ALIYETAMBA YANGA NA SIMBA

Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM

MIAKA ya mwishoni na 80 na mwanzoni mwa miaka ya 90 Saidi Nassoro Yusuph Mwamba ama Kizota alichomoza kwenye soka na kutamba katika vilabu vya Yanga, Simba na timu ya taifa, Taifa Stars.

Kizota alikuwa na uwezo mkubwa wa kusakata kandanda na alisifika kwa magoli ya vichwa, kuna wakati mchezaji huyo alikuwa akicheza kama mshambuliaji na wakati mwingine alicheza kama beki wa kati.

Amewahi kupata heshima akiwa na Yanga ambayo itamfanya asisahaulike kamwe, kwa sasa ni marehemu na alifariki Februali 11 mwaka 2007 kwa ajali ya gari maeneo ya Temeke Vetenary.

Kizota alikuwa anatoka uwanja wa Taifa kuangalia pambano la kombe la Washindi barani Afrika (Sasa Shirikisho) kati ya Simba na Chapungu ya Msumbiji, akiwa njiani aligongwa na gari na kufariki papo hapo.

Kona yetu imeanza kumkumbuka Kizota ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Tabora aliyepata kuzichezea Tindo ya Tabora na CDA ya Dodoma, je wiki ijayo tutakuja na nani? ni jambo la kusubiri

Saidi Mwamba "Kizota" kwa sasa ni marehemu

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA