Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2024

Mtangazaji wa redio ya Alikiba amsifia Diamond

Picha
Mtangazaji wa Crown Fm na Crowntv ya Alikiba Salim Kikeke amempongeza Diamond Platnumz nakumpa heshima kubwa baada ya wimbo wake KOMASAVA kufanyiwa challange na msanii wa Marekani Chris Brown Diamond Platinumz amekuwa na uhasimu na Alikiba, hivyo kitendo cha Kikeke kumsifia Diamond kunaleta tafrani ingawa hilo haliwezi kutokea kwani anayestahili pongezi apewe tu

Vipers yaipora mchezaji Kagera Sugar

Picha
Nyota wa Kimataifa wa Uganda,Dissan Galiwango yupo mbioni kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Vipers ya Uganda. Galiwango alijiunga na Kagera Sugar Mwanzoni mwa msimu 2023-2024 akitokea Vipers ya Uganda,Atarejea Uganda baada ya kulitumikia Jumba la ladha na hekaheka #LigiKuu kwa msimu mmoja pekee.

Samson Madeleke ni mali ya Pamba FC

Picha
Mlinzi wa kati Samson Madeleke amesaini Pamba Jiji FC mkataba wa miaka miwili akitokea Mashujaa FC. Madeleke kabla ya Mashujaa FC alikuwa mlinzi wa Mbeya City ya Mbeya.

Kipre Jr kuuzwa MC Alger

Picha
Azam FC imepokea ofa rasmi kutoka kwa MC Alger ya kutaka kumsajili winga wao raia wa Ivory Coast, Kipré Zunon (24), Imefahamika Azam pamoja na uongozi wa Kipré sasa watasoma ofa hiyo na kufikia uamuzi wa mwisho. Alifunga mabao 10 katika msimu uliomalizika hivi punde.

Yanga na Chama kimeeleweka

Picha
Klabu ya Yanga SC imefikia makubaliano na kiungo wa kimataifa wa Zambia na klabu ya SimbaSC, Clatous Chama ya kumsajili kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mmoja zaidi iwapo atafanya vizuri ndani ya miezi sita (6) ya mkataba wake. Chama mwenye umri wa miaka 32 atapewa dola 150,000 (zaidi ya milioni 380 za Kitanzania) kama ada ya usajili na mshahara wa dola 13,000 (zaidi ya milioni 33 za Kitanzania) kwa mwezi. Pia ameahidiwa kupewa dola 150,000 akiongeza mkataba wa mwaka mmoja.

Omary Omary na Simba kimeeleweka

Picha
Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya kumsajili aliyekuwa Kiungo wa Klabu ya Mashujaa,Omary Omary kwa Mkataba wa Miaka miwili. Omary Omary anakuwa Usajili wa tatu wa Simba kukamilisha kwenye dirisha hili la Usajili baada ya Joshua Mutale na Lameck Lawi ingawa Coastal Union wamerudisha fedha za usajili wake.

Joash Onyango kutimkia Dodoma Jiji

Picha
Na Salim Fikiri Jr Mlinzi wa kati wa Singida Black Stars zamani Ihefu SC Joash Onyango anakaribia kujiunga na walima zabibu wa Dodoma Jiji. Taarifa ambazo hazina shaka yoyote na chanzo chetu cha habari zimetuweka wazi kwamba Onyango raia wa Kenya ambaye aliwahi kuzichezea Gor Mahia ya Nairobi nchini Kenya na Simba SC ya Dar ea Salaam ya Tanzania, atajiunga na Dodoma Jiji msimu ujao. Onyango amekuwa kwenye kiwango kizuri tangu alioojiunga na timu hiyo iliyokuwa ikijulikana kama Singida Big Stars kabla ya kubadilisha jina na kuitwa Singida Fountain Gate na baadaye Ihefu ikauzwa na nusu ya wachezaji wa Singida Fountain Gate wakaingia Ihefu

Clatous Chama aitosa Simba na kusaini Yanga

Picha
Na Ikram Khamees Kiungo mshambuliaji wa Wekundu wa Msimbazi, Clatous Chama raia wa Zambia amegoma kuongeza mkataba kwenye klabu yake na tayari imefahamika kwamba muda wowote anatambulishwa Yanga SC. Habari zenye uhakika kabisa tena bila shaka yoyote zinasema kwamba Chama amekubali kutua Yanga kwa kandarasi ya mwaka mmoja wenye mshahara wa milioni 20 na ada ya usajili milioni 200. Chama amekataa kusaini Simba, kwani hakufurahishwa kabisa na sakata lake lilitokea mwishoni mwa msimu uliopita, Chama anadai anataka kucheza na Khalid Aucho, Stephanie Aziz Ki na Prince Dube. Kwa maana hiyo Yanga itakuwa moto wa kuotea mbali kutokana na majina ya wachezaji hao yalivyokuwa makubwa

Timu ya Job yaichakaza timu ya Kibwana 5-2, Hersi, Dube watupia

Picha
Timu ya beki wa kati wa Yanga SC Dickson Job jioni ya leo imeichakaza timu ya beki wa pembeni wa Yanga pia katika mchezo wa kirafiki uliopewa jina la Wape Tabasamu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Licha kwamba mpira ulikuwa mzuri na wa kupendeza, timu Job ilikuwa ya kwanza kuandika bao kupitia kwa Hersi Said dakika ya 13 kabla ya Said Ndemla dakika ya 23 kuongeza  la pili. Prince Dube dakika ya 26 aliandika bao la tatu, lakini Simon Msuva dakika ya 30 na 47 aliifungia mabao mawili timu ya Kibwana Shomari, George Mpole dakika ya 70 alifunga bao la nne na Samson Mbangula aliweka bao la tano dakika 79 na Edwin Balua dakika ya 90 alihitimisha kalamu ya mabao

Mbappe aishika pabaya PSG

Picha
Kylian Mbappe anatuma barua rasmi kwa Paris Saint-Germain akidai marupurupu na mishahara yake yenye thamani ya hadi €100M. Mchezaji huyo alikuwa amejitolea kutoa €55M, ikiwa ni pamoja na kodi, kwa masharti fulani. Lakini hakuna makubaliano yaliyotiwa saini yaliyofikiwa, bali yalikuwa ni makubaliano ya mdomo tu. Makubaliano hayakukamilika na hali ililipuka mnamo 2024 Nasser Al-Khelaifi alipopata habari kwamba atahamia Real Madrid.

AS Maniema pre- season yao kuweka Avic Town

Picha
Klabu ya AS Maniema Union inatarajiwa kuwasili Nchini Tanzania kwa ajili ya Pre-season Jijini Dar es Salaam huku wakifikia Kigambonni - Avic Town. AS Maniema ndio timu aliyokuwa anaichezea Yanga SC, Maxi Nzengeli, pia ilikuwa njia ya wachezaji wengi waliowahi kutamba Yanga kama Tuisila Kisinda na Fiston Mayele

Coastal Union wameyakanyaga- Magori

Picha
Na Shafih Matuwa Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba SC Crescentius Magori amesema kwamba Coastal Union imeyakanyaga. "Ndio tulichelewa kumaliza pesa,. tulilipa nusu lakini mpaka June tulikuwa tumemaliza kulipa pesa yoye ya usajili" "Tumemsajili Lameck Lawi kwa kufuata utaratibu. Wangesema kama ukichelewa kulipa mkataba unavunjika. Mpaka June tulikuwa tumemaliza kulipa pesa yote na nyaraka zote tunazo hata tukienda FIFA" "Kilichotokea Coastal Union wakapata deal kutoka nje ndio maana wakabadili maamuzi" Amesema Crescentius Magori. Mjumbe wa bodi ya Simba SC.

Imeisha hiyo...Prince Dube ailipa Azam

Picha
Mshambuliaji ambaye ni raia Zimbabwe, Prince Dube amekamilisha kulipa fidia zote alizokuwa akidaiwa na klabu ya Azam ili akatafute changamoto sehemu nyingine. Mshambuliaji Prince Dube anasubiri barua ( Release Letter ) kutoka Azam baada ya kukamilisha malipo hayo, ameshetumiwa ujumbe kuwa atapewa barua hiyo mwanzoni mwa wiki ijayo. Prince Dube anahitaji kubaki Tanzania kucheza moja ya klabu za Kariakoo kuelekea msimu ujao kwenye michuano mbalimbali ya ndani na ya CAF kwa 2024/25.

Coastal Union yarudisha fedha za Lawi, Simba SC

Picha
Klabu ya Coastal Union ya Tanga imerudisha fedha ambazo Simba SC walikuwa wamelipa kwaajili ya uhamisho wa beki wa kati Lameck Lawi. Coastal wamethibitisha kufuta dili hilo wakidai Simba imekiuka makubaliano ambayo yapo kinyume na utaratibu. Jana kupitia mitandao iliweka wazi usajili wa Lawi katika klabu ya Simba lakini baadaye Coastal wakapinga vikali usajili huo

Che Fondoh Malone ataka kuondoka Simba

Picha
Beki wa kati Che Fondoh Malone ameanzisha mtifuano akifosi aondoke ikidaiwa kuwa hana furaha ndani ya Simba SC, utata umeongezeka baada ya Future ya Misri kuonyesha nia ya kumtaka beki huyo aliyejiunga na Simba msimu uliyopita. Viongozi hawataki kumuuza kwani inshu ya Henock Inonga imekaa vibaya, hivyo kuruhusu kuondoka kwa miamba hii miwili itapelekea safu ya ulinzi ya Simba SC kuwa wazi jambo ambalo Klabu hawakujiandaa nalo.

Kumbe Zawadi Mauya ni mwanasheria wa Yanga!!!

Picha
Ni jambo zuri sana Wamefanya Klabu Yanga sc kumuongezea mkataba Mauya, wapo watakao hoji Kwa nini Yeye na Sio Vijana wapya Waingie. Zawadi Mauya kitaaluma ni Mwanasheria ambaye ni Masters Holder, Pia ni mtu ambaye anaisaidia sana Klabu Hususan katika mambo ya Utafsiri wa Sheria hasa Sheria za Michezoni Katika Upande wa Mpira wa Miguu pia ana Verified Certificate Degree in Laws Kutoka FIFA huyu. Yanga wanamuanda endapo akistaafu ataendelea kufanya kazi Yanga SC

Safari Lager Cup kumekuchaa

Picha
Lile tukio kubwa tumekua tukisubiri sasa limefika! Mechi ya fainali ya #SafariCup itafanyika tarehe 29 Juni, viwanja vya Benjamin Mkapa. Ahhha na sii soka kama soka tu bali experience ya kimataifa na performance kali kabisa kutoka kwa Konde Boy @harmonize_tz Endelea kufuatilia kurasa zetu kujua tiketi zinaanza kupatikana lini na wapi maana hii sii ya kukosa.

Nandy amfokea mumewe hadharani

Picha
Msanii Billnass baada ya kumtania mpenzi wake Nandy kuwa anatamani apate mtoto na mdada wa Kenya jibu la Nandy sasa lazua taharuki. Nandy amemjibu tofauti na Bilinas alivyodhani kwani ametoa maneno ambayo yanaonekana kama ya kumfokea. Utani wa wapendanao ni raha sanaa hasa mkiwa mmezoeshana katika utani

Lameck Lawi atambulishwa Simba SC

Picha
Klabu ya Simba Sc imetangaza kumsajili beki wa kati Lameck Lawi (18) kutoka Coastal Union baada ya klabu hiyo kufikia dau linalotakiwa na Coastal Union kwa ajili ya kumuachia Lawi amekuwa akiwindwa na Simba kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho huku kukiwa na taarifa kuwa Henock Inonga yupo njiani kuondoka klabuni hapo.

Magori afanya yake kwa beki la Zesco United

Picha
Mlinzi wa Zesco United, Tandi Mwape raia wa Zambia anatajwa kuwa huenda akajiunga na Simba SC kwenye dirisha hili la usajili. Inaelezwa kuwa Zesco walikuwa kwenye mpango wa kumuongezea mkatabana mazungumzo yalikuwa yanaenda vizuri na nyota huyo lakini ghafla nyota huyo hapokei simu na amekuwa msumbufu. Taarifa za ndani kabisa zinasema kuwa nyota huyo alikutana na kiongozi wa Simba SC ambae alikuwa nchini humo siku kadhaa zilizopita kwa ajili ya mazungumzo na baadhi ya wachezaji wanaohitajika na Lunyasi.

Kennedy Juma naye apewa thank you

Picha
Klabu ya Simba imetangaza kuachana na aliyekuwa Beki wake wa kati,Kennedy Juma baada ya Mkataba wake na Simba kumalizika. Kennedy alijiunga na Simba miaka mitano iliyopita akitokea Singida United na amefanikiwa kubeba mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa na miamba hiyo ya Tanzania.

Yanga, Simba na Azam zajitoa Kagame Cup

Picha
Timu za Simba, Yanga na Azam FC wamewataarifu CECAFA kuwa hawatoweza kushiriki mashindano ya Kagame Cup kutokana na ratiba kutokuwa rafiki kwao. Simba, Yanga na Azam zimepanga kufanya Pre Season nje ya Tanzania na wameshapanga ratiba zao na nchi watakazokwenda kujiandaa.

Simba, Yanga na Azam msituletea utoto wa kuwapa thank you wachezaji wanaoachwa

Picha
Na Prince Hoza ALIANZA kupewa thank you nahodha John Raphael Bocco maarufu Adebayor akafuatia Said Ntibanzokiza au Saido kama anavyojulikana, thank you ziliendelea kwa Shabani Chilunda na Luis Miquissone. Na bado klabu ya Simba kila kukicha inawapa thank you wachezaji wake inaowaacha, kwa maana wapenzi na mashabiki wa soka wa klanu hiyo na wote kwa ujumla wanatakiwa kuwasha data simu zao au kompyuta ili kujua nani anapewa thank you. Huu ni mtindo mpya wa kuwaacha wachezaji ulioanza msimu uliopita ambapo timu ilitaka kuwatema wachezaji wake hutangaza thank you yaani inaachana na mchezaji husika. Kuanzia Simba, Yanga na Azam walianza na staili hiyo ya thank you, kuna baadhi ya mashabiki wa soka wametokea kufurahishwa na staili hiyo ya kuwapa thank you wachezaji wake ilioshindwana naye. Lakini kuna mashabiki wengine hawafurahishwi hata kidogo na staili hiyo, ila najua kwamba Simba, Yanga na Azam zinafanya biashara kwenye akaunti zao za mitandao ya kijamii. Kitendo cha mashabiki wake kunun

Mastaa wa zamani Yanga watembelea Avic Town

Picha
Wachezaji wa zamani wa Klabu ya Young Africans Sports Club leo wamewatembelea na kuzungumza na vijana 22 wa Safari Champions, walioweka kambi AVIC Town kujiandaa na mchezo Maalum wa Safari Lager Cup, utakaopigwa Jumamosi ya June 29, 2024 katika uwanja wa Mkapa, Jijini Dar Es Salaam. Magwiji waliotembelea kambi hiyo leo ni pamoja na Edibily Lunyamila, Kenneth Mkapa, Steven Names, Said Maulid, Omary Hussein na Salvatary Edward.

Ibrahim Ajibu afufua mazungumzo ya kubaki Coastal Union

Picha
Winga Ibrahim Ajibu ameanza mazungumzo mapya na Coastal Union, baada ya kumaliza mkataba wake wa mwanzo msimu ulioisha, wakati huo huo mkononi mwake akiwa na ofa za timu nyingine za Ligi Kuu. . Ukiachana na Coastal Union, timu nyingine zinazotajwa kumpelekea ofa Ajibu ni Namungo, KMC na Kagera Sugar na rafiki wa karibu wa mchezaji huyo, ameeleza anaangalia ni timu yenye maslahi mapana ili asaini. . Staa huyo wa zamani wa Simba, Yanga na Azam ni miongoni mwa wachezaji wenye uzoefu mkubwa kwenye Ligi na ndio sababu kubwa ya makocha mbalimbali kutaka kuwa nae kikosini.

Alikamwe akiri Yanga kudaiwa na FIFA ila sasa safi

Picha
“Ni kweli tulikuwa na tunadaiwa na Mamadou Doumbia, Lazarus Kambole lakini tulikuwa kati kati ya msimu tukaona tujikite kwenye vipaumbele vilivyopo vya klabu kumaliza msimu vizuri na kuchukua makombe, jambo ambalo tumefanikiwa” Ali Kamwe Meneja wa Habari na Mawasiliano Yanga Sc. “Baada ya msimu kukamilika tuka ‘clear’ madeni yote tuliyokuwa tunadaiwa. Kabla ya Dirisha la usajili kufunguliwa sisi Yanga tulikuwa tumeshafanya malipo yote kwa 100% ya hawa wachezaji wawili.” “Juni 14, 2024 tulituma Proof Of Payment FIFA na Jana, Juni 18 tulipokea Email kutoka FIFA kwamba wamejiridhisha na malipo yetu.” “Kwa taarifa rasmi ni kwamba hakuna kesi yoyote FIFA inayohusisha Young Africans, jambo la Okrah muda ukifika litakuja kuzungumzwa kulingana na ripoti ya mwalimu mwenyewe kama atabaki au ataondoka,” — Ali Kamwe kupitia Wasafi FM.

Mgunda huyoo Mashujaa

Picha
Na King David Paschal Ismail Mgunda amejiunga na Mashujaa Kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Singida Black Stars Mgunda alijiunga na Singida Black Stars zamani Ihefu fc akitokea Tanzania Prisons mwaka Jana mwezi Julai

Luis Miquissone aungana na Saido

Picha
Klabu ya Simba SC imeachana na aliyekuwa Kiungo Mshambuliaji wake,Luis Miquissone kufuatia kiwango kibovu alichoonyesha nyota huyo tangu amesajiliwa na Simba kwa mara ya pili. Miquissone hajafunga goli lolote akiwa na Simba ndani ya Mechi 19 alizocheza huku akitoa assist 4 pekee. Jana mtandao huu uliandika kwamba Miquissone ataendelea kusalia kwenye kikosi hicho, lakini leo klabu yake ya Simba imempa thank you.

Augustine Okrah apewa thank you Yanga

Picha
Ni rasmi, Augustine Okrah hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao. Baadhi ya viongozi wa Yanga SC walitaka Okrah abaki lakini kocha Miguel Gamondi amewaambia kuwa, Okrah hayupo kwenye mipango yake, Yanga ichague kati ya Gamondi na Okrah, nani abaki !. Okrah amevunjiwa mkataba rasmi, amerejea katika klabu aliyotoka, Bechem United. Okrah na wanasheria wake wamesema wataipeleka Yanga SC (FIFA) ikiwa hawatawalipa pesa wanazodai.

Baada ya kumalizana na Mutale, Simba kushusha kiungo mkabaji

Picha
Baada ya kudaiwa kumalizana na Joshua Mutale kutoka Zambia, mabosi wa Simba wameanza kumfuatilia kiungo mkabaji wa Rivers United, Augustine Okejepha (20) ili atue kuiboresha timu hiyo msimu ujao. . Kiungo huyo inadaiwa anaonwa ni chaguo sahihi Simba kwa ajili ya msimu ujao, japo timu mbalimbali zimeonyesha kuvutiwa naye ikiwemo, FC Ural ya Urusi inayoshiki Ligi Daraja la Kwanza.

Saido Ntibanzokiza atupiwa virago Simba

Picha
Kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza hatokuwa sehemu ya kikosi cha Simba kwa ajili ya msimu wa 2024/25 baada ya kumaliza mkataba wake. . Taarifa iliyotolewa mapema leo, Saido hatoonekana msimu ujao kwenye kikosi cha Simba ingawa alikuwa kwenye msimu bora, hasa wa 2022/2023 ambapo aliweza kuwa mfungaji bora. Hata hivyo Saido anatajwa kujiunga na Coastal Union ya Tanga ambao nao watashiriki kombe la Shirikisho barani Afrika msimu ujao ambapo Simba nao watashiriki michuano hiyo hiyo

Job amuomba radhi kocha wa Stars

Picha
Beki wa Klabu ya Yanga Dickson Job amemuomba Radhi Kocha wa Taifa Stars Ahmed Morroco Kufuatia Kutoelewana Kwao Jambo lililopelekea Dickson Job kutoitwa Katika Kikosi cha Stars Kinacho wania Kufuzu Kombe la Dunia 2026. Dickson Job amekuwa na Mgogoro na Kaimu kocha Mkuu wa taifa Stars Ahmed Morroco Akihusishwa na Kugomea Kucheza Katika Michuano ya Afcon2023 (Ivory Coast) pia Ikisemwa Dickson Job alipewa Majukumu na Mwalimu wake huyo Kucheza Namba Fulani na Kisha yeye akakataa. Dickson Job Kupitia Kipindi cha #KipengaExtra cha East Africa Redio na East Africa TV kwa Mara ya Kwanza Dickson Job anakanusha Madai hayo yaliyopelekea Mpaka Kuonekana sio Mzalendo wa taifa lake. Dickson Job anasema yeye hajawahi Kugomea Majukumu aliyopewa na Mwalimu huyo na Kuhusishwa na Kugomea Taifa Lake Jambo ambalo sio Kweli. Yote kwa yote Dickson Job ametumia Nafasi hiyo Kumuomba Radhi Mwalimu wake Ahmed Morroco na Kuwaomba Radhi Watanzania ambao walikwazika kwa namna moja hama Nyingine Baada ya Kusikia Uvu

Luis Miquissone kusalia Simba

Picha
Luis Miquissone ataendelea kusalia katika klabu ya Simba SC baada ya mazungumzo ya kuvunja mkataba kushindikana. Miquissone alirejeshwa katika klabu hiyo.akitokea Al Ahly ya Misri alikosajiliwa msimu wa 2021/2022 akitokea Simba SC akiwa kwenye kiwango bora. Hata hivyo kiwango chake kimeshuka na sababu kubwa ikitajwa kuwa ni uzito ambapo kiungo mshambuliaji huyo kunenepeana na kumfanya ashindwe kuonyesha uwezo wake kama aliokuwa mwanzo. Inadaiwa kwamba analipwa milioni 45 kwa mwezi, ambapo Simba inataka imtoe kwa mkopo, lakini wasimamizi wake wamekataa na pia mpango wa kuvunja mkataba nayo imeshindikana

Edna Lema kurejea Yanga Princess

Picha
Klabu ya Young Africans imefanya mazungumzo na aliyekuwa kocha wao wa Yanga Princess Edna Lema ili kurejea klabuni hapo. Edna Lema ana mkataba wa mwaka mmoja wa Biashara Utd kama kocha msaidizi unakaribia kumalizika mwezi huu.

Yanga kuanza kumtambulisha Prince Dube

Picha
Maandalizi juu ya kumtambulisha mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe Prince Mpumalelo Dube kwenye klabu ya Yanga- yameanza sasa. Mmoja kati ya mtu wa karibu wa klabu hiyo ameitonya Mambo Uwanjani Blog kuwa Yanga inataks kumtambulisha Dube muda wowote hivyo mashabiki wao wakae mkao wa tayari. Dube alikuwa anaichezea Azam FC na aliamua kuvunja mkataba wake hasa baada ya kutoridhishwa na hali ya mambo, na Yanga- imekuwa timu pekee iliyomvutia na akitaka kujiunga nayo

H Baba ajiweka shakani kwa Harmonize

Picha
Mwaka jana/juzi H Baba alijitoa kwenye uwanafamilia wa Konde Gang ya Harmonize na kuhamia Wasafi family ya Diamond Platnumz, baada ya kuondoka kwa Harmonize alitoa maneno mengi machafu na udhalilishaji huku akimsifia Diamond Platnumz kwa kumuomba msamaha na kumsujudia miguuni. Baada ya mambo kwenda ndivyo sivyo tofauti na matarajio yake, familia ya Diamond imekuwa ikionyesha kutokuwa na muda nae, kumnyima upenyo wa kula chungu kimoja. H Baba ameamua kurejea kwenye kambi yake ya awali ya Konde Gang na bila hiyana Harmonize amempokea kwa mikono miwili baada ya kumpigia magoti na kujutia maamuzi yake ya kuisaliti kambi ya Konde Gang.

Jobe gumzo kila kona

Picha
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinaeleza kuwa baadhi ya vilabu kutoka nchi mbalimbali vimegonga hodi Msimbazi zikihitaji huduma ya mshambuliaji wa Simba Pa Omar Jobe kwenye dirisha kubwa la usajili. Pa Omar Jobe hakubahatika kuwa na msimu mzuri kwenye timu hiyo baada ya kusajili kwenye dirisha dogo akichukua nafasi ya Moses phiri ambapo alifanikiwa kufunga goli moja ligi kuu na goli moja kwenye michuano ya Cafcl.

Simba yampa thank you John Bocco

Picha
Klabu ya Simba imempa mkono wa kwaheri aliyekuwa kiongozi wa wachezaji (nahodha) John Raphael Bocco ikiwa alijiunga na klabu hiyo akitokea Azam FC. Kwa niaba ya Wanasimba Bocco anastahili kupewa sifa ya pekee na atakumbukwa zaidi kwani rekodi zake alizoweka ni kubwa sana na Simba inakutakie mafanikio mema katika majukumu yako baada ya soka.

Dodoma Jiji yawasajili Luhende, Seseme

Picha
Taarifa nilizonazo muda huu:Klabu ya Dodoma Jiji imekamilisha usajili wa nyota wawili Abdallah Seseme pamoja na David Luhende kutoka Kagera Sugar. Nyota hao wawili wamekuwa na wakati mzuri sana kwa misimu mingi ambayo wamekuwa wakiitumikia Kagera Sugar.

Bodi mpya ya wakurugenzi Simba SC hii hapa

Picha
Wajumbe walioteuliwa na Mohamed Dewji maarufu Modewji kuwa wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Simba SC upande wa Mwekezaji. Waliochaguliwa ni Cresentius Magori, Hussein Kita, Salim Abdallah Tryagain, Mohamed Nassoro, Zulfikar Chandu na Rashid Shangazi Try Again, Shangazi na Zulfikar walikuwemo kwenye bodi ya wakurugenzi iliyojiuzuru hivi karibuni kabla ya kurejeshwa tena chini ya Modewji

Diva The Bawse anahitaji kidume cha kumdekeza

Picha
Mtangazaji maarufu Diva the bawse baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake Abdul sasa ametangaza kuwa Jimbo liko wazi anatamani kumpata mwanaume atakayeweza kumdekeza. Diva The Bawse ambaye kwa sasa ni mtangazaji wa Wasafi FM amesema hayo hivi karibuni ambapo anadai anatamani kupata kidume kitakachoweza kumdekeza. "Natamani kudeka, mimi ni mwanamke napenda sana kudeka hasa kwa mwanaume anayejua mapenzi, kudeka ni haina ya staili zetu walimbwende kwa sisi" alisema staa huyo wa mtangazaji Tanzania

Tabora United yabaki Ligi Kuu bara

Picha
Timu ya Tabora United ya Mkoani Tabora imefanikiwa kubaki katika Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Biashara United ya Mara, ambapo jumla ya matokeo ni magoli 2-1 kwa kuwa mchezo wa kwanza Biashara ilishinda goli 1-0 Mchezo huo wa “Play Off” umepigwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi. Biashara itaendelea kubaki katika Ligi ya Championship msimu ujao wa 2024/25

Nyota Chelsea atoa maboksi ya viatu na nguo zake kwa watoto wa mitaani Senegal

Picha
Nyota wa Klabu ya Chelsea na timu ya Taifa ya Senegal, Nicolaus Jackson ametoa maboksi 20 yenye viatu na nguo alizotumia kwenye Msimu wake wa kwanza akiwa na Chelsea kwa watoto wa mtaani kwao Senegal ikiwa ni sehemu ya kutimiza falsafa inayosema upendo huanzia nyumbani.

JKT Tanzania yafuta benchi lote la ufundi

Picha
JKT Tanzania FC imeifuta kazi benchi lao lote la ufundi ambalo lilikuwa linaongozwa na kocha wake Malale Hamsini ambaye nae ni miongoni mwa waliotumuliwa. Haijajulikana sababu pekee iliyopelekea Malale kutimuliwa lakini Inasemekana kwamba uongozi wa JKT Tanzania haujafurahishwa na timu hiyo kunusurika kushuka daraja na ikiwa ilikuwa ina wachezaji wazuri

Mbwana Makata abadili gia angani, atua Prisons

Picha
Kocha Mbwana Makata amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Tanzania Prisons akichukua nafasi ya Ahmad Ally. Makata akeshasaini mkataba siku ya jana, na sasa viko vitu vichache vinakamilishwa ili aweze kutangazwa kama kocha mkuu wa klabu hio. Kwa mujibu wa taarifa nilizonazo ni kuwa haijafahamika kama ataenda na msaidizi wake atasaidiwa na Kazumba & Mtupa ambao ni makocha wasaidizi Tanzania Prisons.

Philipe Kinzumbi aitosa Yanga na kutimkia Morocco

Picha
Winga wa kimataifa wa DR Congo,Phillipe Kinzumbi amejiunga na Klabu ya Raja Casablanca kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya TP Mazembe ya DR Congo. Kinzumbi ilikuwa asajiliwe na Yanga SC ya Tanzania na ilisemekana kwamba Yanga itabadilishana na Kennedy Musonda lakini dili hilo limeota mbawa kwani ametimkia Morocco

Kipa wa Miliwall afariki akiwa na miaka 26

Picha
Klabu ya Millwall inayoshiriki Ligi daraja la pili Nchini England ya Championship imetangaza kifo cha aliyekuwa golikipa wake, Matija Sarkic raia wa Montenegro ambaye amepoteza maisha akiwa na umri wa miaka 26 Sarkic ambaye ameichezea Millwall jumla ya mechi 33 tangu alipojiunga nayo Agosti 2023 akitokea Wolverhampton. Amewahi pia kuvitumikia vilabu vya Villa, Birmingham City, Stoke City na Timu ya taifa ya Montenegro.

Wachezaji Yanga Princess wamuaga nyota wao Mmarekani

Picha
Baada ya mchezo wa mwisho Ligi Kuu ya Wanawake wachezaji wa Yanga Princess walitumia nafasi ya kumuaga na mchezaji mwenzao Dada Kaeda anaerejea nchini Marekani kuendelea na masomo yake baada kuitumikia Yanga Princess kwa msimu mmoja. Wachezaji wa Yanga Princess hawakufurahishwa kuondoka kwa Kaeda kwakuwa tayari walishazoeana naye na kumfanya kama ndugu yao, hivyo akiwa Marekani wanajihisj watakuwa wapole. Hata Dada Kaeda naye amesikitishwa kuondoka kwake ingawa ni wajibu kuongeza elimu