Azam kumrudisha Tepsie Evance
Azam FC inadaiwa ipo mbioni kumpa nafasi nyingine winga Tepsie Evance (21) baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo kwa KMC.
Baadhi ya viongozi wa timu hiyo wanahitaji kumbakisha Tepsie aliyekulia kwenye akademi yao.
Licha ya kuwa na shutuma za utovu wa nidhamu na sasa dili hilo linasubiri baraka za Kocha Youssouph Dabo kuamua.