Stand United yaipora mchezaji Coastal Union
Timu ya Stand United inayoehiriki Ligi ya Championship imeingia rada za Coastal Union na kumpora kiungo mshambuliaji aliyetajwa kutua kwao Abdul Machela na kutaka kumpa kandarasi ya miaka miwili.
Machela ambaye kwasasa yupo nchini Msumbiji akicheza kwenye klabu ya Black Bulls inayoshiriki Ligi daraja la kwanza huenda akarejea Tanzania kujiunga na Stand inayonolewa na Seleman Kitunda.
Machela ni mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa Wekundu wa Msimbazi, Simba SC Ally Machela, amekubali kutua Stand United ingawa dili lake na Coastal Union lilikaribia kuiva ila kocha wa Stand, Kitunda amesema Machela ni mchezaji mzuri atawasaidia kupanda Ligi Kuu msimu ujao