Augustine Okejepha miaka miwili Msimbazi
Klabu ya Simba SC imefikia makubaliano ya kumsajili wa Kiungo Mkabaji wa Kimataifa wa Nigeria na Klabu ya Rivers United inayoshiriki Ligi Kuu Nchini Nigeria, Augustine Okejepha kwa Mkataba wa Miaka mitatu.
Kwenye makubaliano na Klabu yake ya Rivers United inaonesha Kiungo huyo mwenye umri wa Miaka 20 amenunuliwa na Simba kwa kiasi cha Shilingi Milioni 515 za Kitanzania na atakuwa anapokea Mshahara wa Shilingi Milioni 16 kwa Mwezi ambayo ni mara 10 na Mshahara wake aliokuwa anaupata Rivers.
Fundi huyo wa mpira atatua Tanzania wiki ijayo kwaajili ya kusaini Mkataba na Miamba hiyo ya Tanzania.