Ajibu amfuata Ndemla, Bocco JKT Tanzania
Kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu Migomba amejiunga na JKT Tanzania baada ya kumaliza mkataba wake Coastal Union ya Tanga.
Ajibu aliyewahi kuzichezea Simba na Yanga zote za Dar es Salaam, bado hakuwa kwenye msimu mzuri tangu alipojiunga na Azam FC, Singida Fountain Gate na Coastal Union.
Akiwa JKT Tanzania, Ajibu atakutana ns maswahiba zake Said Ndemla, Shiza Kichuya na John Bocco aliowahi kukutana nao Simba SC