Simba yabariki Inonga kwenda FAR Rabat
Klabu ya Simba SC imekubali kumwachia beki wao wa kimataifa wa DR Congo, Henock Inonga Baka aliyebaki na mkataba wa mwaka mmoja kwenda klabu ya FAR Rabat yavMorocco inayoshiriki Ligi Kuu nchini kwa dau la dola 200,000 (Milioni 525 za Kitanzania).
Inonga alisaini FAR Rabat wakati Ligi Kuu bara ikiendelea na alijitoa kikosini na kwenda Ufaransa huku akidai kwamba mkataba wake na Simba umeisha, lakini Simba yenyewe imekuwa ikigoma na kudai bado ina mkataba naye wa mwaka mmoja