Coastal Union waanza usajili kwa kishindo
WAGOSI wa Kaya wapo bize na maandalizi ya msimu ujao wa mashindano, hususani Kombe la Shirikisho Afrika na kwa sasa imeanza mazungumzo na kiungo mshambuliaji Mkenya Duke Abuya anayekipiga Singida Black Stars (zamani Ihefu).
.
Nyota huyo inaelezwa huenda akaondoka kikosini humo baada ya mkataba aliokuwa nao Ihefu kumalizika, huku kukiwa hakuna mazungumzo mapya ya kumuongezea, japo timu ya Polisi Kenya aliyokuwa akiichezea kabla ya kuja nchini.
Inatajwa kutaka kumrejesha, huku uwepo wa kocha David Ouma ulitajwa chanzo cha kumvuta Coastal Union hasa kama mazungumzo baina yao yatamalizika freshi.