Yanga yaingia mkataba na Safari Lager

MABINGWA wa soka nchini, Yanga wameingia makubaliano na Kampuni ya bia nchini (TBL) kucheza mchezo maalum na kikosi cha Safari Champion Juni 29 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Ikumbukwe TBL iliendesha mashindano maalum ya kusaka vipaji na kuchagua wachezaji waliounda timu hiyo ya Safari Champion.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Yanga, Andrew Ntime, alisema makubaliano hayo yatasaidia kuinua vipaji vya vijana ambao watazitumikia timu za Taifa hapo baadaye.

"Hii ni fursa ya pekee kwetu kuingia makubaliano na kampuni hii katika kuhakikisha tunaibua vipaji vya vijana ambao hapo baadaye watazitumikia timu za Taifa," alisema Mtime.

Kwa upande wake Meneja wa chapa wa TBL, Pamela Kikalu, alisema timu hiyo ya Safari Champion ina jumla ya wachezaji 22 ambao wamepatikana katika mikoa minne ya Tanzania Bara, kupitia mchakato wao uliaoanza mwezi Agosti mwaka jana.

"Mchakato huu ulianza tangu mwezi Agosti kwa kukusanya vijana zaidi ya 1,000 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara ambao tuliwafanyia mchujo na kupata idadi hii," alisema Kikalu.

Alisema mbali na tamasha hilo vile vile kutakuwa na burudani zitakazotolewa na wasanii Harmonize wa Tanzania pamoja na Koffi Olomide kutoka Kongo


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA