Rich Mavoko adai alikaa kimya sababu alizuiliwa na mahakama
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Rich Mavoko ameweka wazi kwa mara ya kwanza sababu zilizopelekea kukaa kimya kwa muda mrefu bila kujishughulisha na kazi za muziki.
Staa huyo akiwa kwenye mahojiano kwenye kipindi cha XXL cha Clouds Fm amesema kuwa alipata kesi ya madai na moja ya kampuni kubwa ya kusambaza kazi za wasanii.
'Nilipitia changamoto kidogo ya kesi ya madai japo kuwa mimi ndiye nilikuwa nadai lakini niliambiwa nitulie kwanza mpaka kesi iishe"