Tumesajili wapya 7- Ahmed Ally
Meneja wa habari wa Wekundu wa Msimbazi, Simba SC Ahmed Ally amesema kwamba Simba tayari imesajili wachezaji 7 wapya wa kimataifa.
"Niwahakikishe wanasimba kuwa "Thank you" bado zinaendelea, hizo zilizotoka ni chache kuliko zilizobaki, Tunataka kombe la msimu ujao lije Msimbazi. Hivi sasa viongozi wa Simba wanapishana angani kutafuta wachezaji bora"
"Msishangae kuona Thank you zinachelewa ni kwasababu tuliopanga kuwapa kuwaacha bado wanamikataba, hatutaki kuwa kuingia kwenye rekodi ya FIFA ya wadaiwa sugu. Usajili unaendelea tumeshasajili wachezaji 7 ambao tayari wameshatua hapa nchini" Ahmed Ally.