Mrithi wa Benchikha kutangazwa wiki hii
Hivi karibuni klabu ya Simba SC inatarajiwa kumtangaza kocha Steve Komphela raia wa Afrika Kusini ambae anakuja kuchukua nafasi Abdelhak Benchikha ambae alivunja mkabata na miamba hiyo ya Msimbazi.
Kocha huyo wa zamani wa Kaizer Chiefs na Mamelod Sundowns za Afrika ya Kusini, anatarajia kutangazwa kama Kocha mkuu wa klabu ya Simba kwa ajili ya Kuwanoa Wekundu wa Msimbazi Msimu ujao.