Baleke adai alishindia maji ya moto na sukari, Simba
Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Simba SC Jean Baleke raia wa DR Congo amesema alipokuwa anaichezea Simba hakuwa na furaha kwani wachezaji wawili tu alikuwa anaongea nao.
Baleke aliwataja wachezaji hao kuwa ni Kibu Denis Prosper na Israel Mwenda, pia amedai kwamba maisha hayakuwa mazuri kwenye klabu hiyo kwani alishindia maji ya moto na sukari.
"Nikiwa Simba usiku nilikuwa nakunywa maji ya moto na Sukari hakuna Chakula, pale simba naongea na watu wawili tu, Kibu Denis na Israel Mwenda."