Manula arejea Azam kwa mkopo
Mlinda mlango nambari moja wa.Tanzania Aishi Manula amesajiliwa na Azam FC kwa kandarasi ya mkopo wa miezi sita kutokea Simba SC.
Manula hakuwa na nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Wekundu hao wa Msimbazi hivyo itakuwa vizuri kwake kwenda kujiimarisha na kulinda kiwango chake.
Pia Azam FC nayo imeamua kumrejesha Manula kwakuwa itaachana na makipa wake wawili wa kigeni Ahmada na Idrisu, hivyo itabakiwa na Mustapha, kwahiyo Manula atakuwa msaada