Simba Day sasa ni Agosti 3
Klabu ya Simba SC imetangaza tamasha lake la Simba Day litafanyika Agosti 3 mwaka huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na linepanga kucheza na timu ya APR ya Rwanda.
Katika tamasha hilo Simba SC itatumia nafasi hiyo kutambulisha kikosi chake chote pamoja na kocha wake mkuu kama ilivyo desturi yake kila msimu kuadhimisha tamasha hilo