Rasmi, Chama, Kanoute, Babacar na Jobe wapewa thank you
Taarifa zilizovuja muda huu ambapo Mambo Uwanjani Blog imejukishwa ni kwamba wachezaji wanne wa kimataifa wa Simba SC skiwemo Clatous Chota Chama "Mwamba wa Lusaka" wamepewa thank you.
Mtoa taarifa wetu ameyaweka wazi majina ya nyota hao na nchi wanazotoka kuwa ni Clatous Chama raia wa Zambia, Pah Omar Jobe raia wa Gambia, Sadio Kanoute raia wa Mali na Babacar Sarr raia wa Senegal.
Chama anatajwa kusajiliwa na watani zao Yanga SC wakati Kanoute anatajwa kutaka kuondoka huku Jobe na Babacar hawajawafurahisha mashabiki wa timu hiyo