Hatufanyi usajili kwa presha ya watu- Magori

MJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Crescentius Magori ameweka wazi kuwa ujio wake ndani ya kamati hiyo imezaa kelele na kuleta hofu kwa wapinzani wao.

Kauli hiyo ni baada ya uwepo wa tetesi nyingii juu ya kiungo Clatous Chama pamoja na mipango ya usajili inayoendelea ndani ya klabu hiyo katika kuimarisha kikosi chao kwa msimu wa 2024/25 wa mashindano.

Kwa mujibu wa Magori amesema wamejipanga vizuri katika usajili na maboresho ya kikosi chao kwa kufanya usajili kulingana na mahitaji ya timu yao kwa kufuata mapendekezo ya benchi la ufundi.

Amesema hawafanyi usajili kwa presha inayofanywa na wapinzani wao, mchezaji ambaye wanamlilia kila mwaka anemleta akiwemo na wengine ambao wamekuja kuwa gumzo Afrika.

“Tupo makini sana, kelele zao zinaashiria hofu juu ya uatari wangu, ndio kwanza tumeanza na tunafanya usajili mkubwa kwa kuimarisha kikosi chetu bila ya presha za watu.

Wanasimba wasiwe na wasiwasi kabisa, sio mgeni katika usajili nimekuwa kwenye nafasi hii misimu minne yote Simba ilikuwa bingwa, sio ubingwa tu tulifanya makubwa Afrika mpaka kuingia katika 10 bora ya timu tishio Afrika,” amesema Magori.

Amewaomba mashabiki kuondoa wasiwasi juu yanayoendelea anaamini ni figisu zinazoendelea juu ya usajili wa beki Lameck Lawi, wapo makini na viongozi wenzake kwa lengo la kurejesha heshima ya klabu hiyo.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA