Lawi ni mchezaji wetu- Ahmed Ally
Afisa habari wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema Coastal union wanajisumbua kuwarudishia pesa za usajili za mchezaji wao Lameck Lawi kwani wao kama Klabu,walifuata taratibu zote za kisheria na mkataba upo
Alikuwa Instagram live, akijibu maswali mbali mbali ya mashabiki wa Klabu hiyo ndipo akaulizwa kama kweli pesa za usajili wa mchezaji huyo zimerudishwa,ikimaanishwa kwamba,Coastal hawataki kuwauzia
"Wamerejesha,hawajarejesha lakini as long as wali saini mkataba na Simba SC na wakakubali kumuuza mchezaji wakahitaji hiyo fedha na wakalipwa hiyo fedha,hiyo kurudisha ni kujisumbua tu
La muhimu ni kwamba makubaliano yapo,makubaliano halali na kila kitu kimefuatwa kama kilivyo kwenye makubaliano,hilo la kurudisha fedha na nini wala lisiwatie mashaka ndugu zanguni wana Simba tulieni".