Ivo Mapunda atozwa faini kwa kummwagia maji mchezaji wa Tabora United
Kocha wa magolikipa wa Klabu ya Biashara United, Ivo Mapunda, ametozwa faini ya Tsh. 500,000,/= Kwa kosa la kummwagia maji mchezaji wa Tabora United alipokua akitoka uwanjani Kwa mwendo wa pole Hali iliyotafsriwa kuwa ni kupoteza muda.
Tukio hilo lilitokea Kwenye mchezo wa play off ambapo timu hizo zilikutana huku moja ambayo ni Tabora United ikitafuta kusalia ligi kuu ya NBC huku Biashara United ikitafuta tiketi ya kurejea kwenye ligi kuu ya NBC msimu wa 2024/2025.
Katika michezo hiyo ya Play off, Tabora United ilifanikiwa kushinda na kusalia kwenye ligi kuu ya NBC.