Mzamiru, Mwenda wapewa miaka miwili Simba
Kiungo mkabaji wa Simba, Mzamiru Yassin amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia Msimbazi.
Mkataba wa Mzamiru umemalizika mwishoni mwa msimu huu na mapendekezo ya kiufundi yamependekeza mchezaji huyo kubaki kutokana na mchango wake.
Hivyo uongozi wa Simba umemuongezea miaka mingine miwili ya kuendelea kusalia kikosini, pia Simba imemuongeza mkataba wa miaka miwili beki wake wa pembeni Israel Mwenda.