Buriani Yusuph Manji
Aliyewahi kuwa mfadhili wa Klabu ya Yanga SC na Mkurugenzi wa Quality Group Limited (QGL) Bilionea Yusuf Manji amefariki dunia leo, Juni 30, 2024.
Yusuph Manji amefariki dunia akiwa Marekani alipokuwa akipatiwa Imatibabu.
Manji atakumbukwa sana na wapenzi wa soka nchini kwani amechangia kwa kiasi kikubwa kukuza ligi yetu na kuimarisha Yanga na Simba hasa aliposaidia wachezaji kulipwa mishahara.
Mambo Uwanjani itawaletea simulizi mbalimbali za bilionea huyo, Mungu amlaze mahara pema, peponi, Amina