Kikwete ashangazwa na miujiza ya bonde la ufa na riadha
Rais mstaafu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete ameshangazwa na wanariadha kutoka bonde la ufa kuibuka washindi wa mashindano mbalimbali.
Akizungumza na Wasafi FM katika kipindi cha Good Morning, Kikwete amesema kwamba mchezo wa riadha ni wa ajabu sana kwani washindi wote wa riadha kuanzia hapa nchini na Kenya wanatokea bonde la ufa.
"Kuanzia Filbert Bayi na Juma Ikhangaa wanatokea eneo la bonde la ufa, hata washindi wanaotokea Kenya wote wanatoka bonde la ufa, nashangaa sijui kuna nini kati ya riadha na bonde la ufa", alisema Kikwete ambaye alikuwa Rais wa awamu ya nne