George Mpole akana kusaini Yanga
Aliyekuwa mshambuliaji wa FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Klabu ya Geita Gold, George Mpole, amesema bado hajasaini Timu yoyote licha ya kupokea ofa nyingi kutoka Klabu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
Baada ya taarifa kuwa mshambuliaji huyo amemalizana na uongozi wa Yanga kwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo kwa msimu wa 2024/25, Mpole amesema tayari amepokea ofa nyingi ikiwemo Yanga.