Simba kuibomoa Yanga kwa Mwamnyeto
Simba ipo kwenye mazungumzo ya "u-serious" na kambi ya mlinzi tegemezi wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto ili kuona uwezekano wa kumsajili ifikapo mwishoni mwa msimu huu ambapo mchezaji huyo atakuwa huru kujiunga na timu yoyote ikiwemo Simba
Mnyama amefikia hatua hiyo baada ya kuwa mbele zaidi kwa hatua kadhaa kutokana na kusuasua kwa dili lake jipya kunako kikosi cha Yanga hivyo fasta mabosi hao wameamua kuitaka saini yake ukiwa ni muendelezo wa kuongeza ubora kwenye kikosi chao ambacho huenda kikawa na mapungufu makubwa kwenye eneo la nyuma ikihusishwa kuondoka kwa Inonga pamoja na Kennedy Juma baada ya msimu huu kuisha
Msimu huu Mwamnyeto amekuwa mtu wa kiungia kikosini na kutoka huku mwalimu akiwaamini zaidi Ibrahim Bacca pamoja na Dickson Job na huenda hilo limekuwa kama ishara ya kuwa Nondo hatokuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kwa msimu ujao