Straika la mabao Asante Kotoko kusaini Simba Ijumaa
Mshambuliaji wa Asante Kotoko na timu ya Taifa ya Uganda, Steven Mukwala yupo kwenye hatua ya mwisho kabisa ya mazungumzo na klabu ya Simba SC.
Ijumaa hii mchezaji huyu Mukwala atasaini mkataba wa miaka 3 kuitumikia Simba SC.
Mukwala atalipwa kiasi ya dola $130,000 takribani shillingi 327,600,000 fedha ya Tanzania kama ada ya usajili.
Aidha mchezaji huyo atapokea kiasi cha dola $9,000 sawa ni shillingi 22,680,000 fedha ya Tanzania kama mshahara wa kila mwezi.