Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2016

HATIMAYE ZILE T: SHIRT ZA KIJANJA ZINAPATIKANA MADUKANI

Picha
Na Saida Salum, DAR ES SALAAM HATIMAYE zile tisheti za kijanja zilizobuniwa na mbunifu chipukizi wa mavazi Ndulumo Junior Mbazi zimeanza kusambazwa madukani hapa jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Mtandao huu, Ndulumo Junior amesema tayari tisheti zake zenye maneno mbalimbali ya kufurahisha yakiwemo 'UsI4c Nikuamini' zimeanza kusambazwa madukani. Tisheti hizo zinapatikana katika maduka kadhaa Kariakoo na nyingine zipo Tabata Da West kwenye saluni ya kike ya mwanadada Veronica Mdamo na pia katika stationary ya Salma iliyopo Tabata Mtambani karibu na kwa mzee Njalangi. Waweza pia kumpigia simu yake 0713690868

NGOMA AIPASUA KICHWA YANGA

Picha
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga SC  Donald Ndombo Ngoma raia wa Zimbabwe anaipasua kichwa klabu hiyo baada ya kugoma kuongeza mkataba mwingine. Ngoma amekataa kuongeza mkataba mwingine hasa baada ya kugundua kuwa Yangs hawako tayari kumuuza, Ngoma alitakiwa nchini Australia lakini Yanga waliikalia ofa hiyo. Na sasa anatakiwa nchini Afrika Kusini lakini pia klabu yake haionyeshi nia yoyote ya kufanya mazungumzo na timu hiyo, hivyo ameamua kutoongeza mkataba ili huu wa sasa unaotarajia kumakizika mwakani uwe wa mwisho kwake. Ngoma alitua Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea FC Platinum ya Zimbabwe na hadi amekuwa tegemeo katika kikosi hicho chs Yanga, Naye msemaji wa Yanga Jerry Muro amezikana taarifa hizo na kudai hakuna klabu yoyote iliyotuma ofa Yanga ya kumuhitaji mshambuliaji huyo Ngoma amegoma kuongeza mkataba mpya Yanga

KIPRE TCHETCHE ASAINI AL NAHDA YA OMAN, AZAM WAHAHA

Picha
Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Azam FC raia wa Ivory Coast amesaini mkataba wa kuichezea Al Nahida ya Oman na sasa ameachana rasmi na Azam. Taarifa zilizoenea leo zinasema mshambulizi huyo pia anawindwa na mabingwa wa soka nchini Yanga SC, Tchetche ni mmoja kati ya washambuliaji bora kabisa waliokinukisha katika ligi kuu ya bara na ni miongoni mwa wachezaji walioipa ubingwa wa bara mwaka juzi. Hata hivyo viongozi wa Azam wamekuja juu wakitaka suala la mchezaji kulifikisha FIFA  kwani wanadai Tchetche bado ni mali na ana mkataba wa kuitumikia timu hiyo

BMT, TFF MNATAKA KUIPELEKA WAPI YANGA?

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) lilipokea agizo kutoka Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Wasanii la kutaka vyama vyote vya michezo na vilabu ambavyo havijafanya uchaguzi vifanye haraka ifikapo Juni mwaka huu. Waziri wa wizara hiyo Nape Moses Nnauye alikuwa mstari wa mbele kuvitaka vilabu na vyama kuchaguana kwa njia ya kidemokraisa, BMT ililigeukia Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF na kulitaka liwaambie wanachama wao ambao hawajafanya uchaguzi wafanye haraka mwaka huu. Yanga SC ikakutwa na hatia kwani haijafanya uchaguzi wake kisheria tangu mwaka 2014 ambapo muda wa uongozi wao ulifikia tamati, hata hivyo wanachama wa klabu hiyo walimuongezea muda zaidi nwenyekiti wao Yusuf Mehbood Manji kwa kipindi cha mwaka mmoja. Manji aliendelea kukaa madarakani kwa mwaka mmoja zaidi na makubaliano yao wafanye uchaguzi mwaka jana 2015, lakini nao pia hawakufanya tena uchaguzi na kisingizio kikubwa ni uchaguzi mkuu wa nchi ambao ulifanyika Oktoba 25, 201...

HANSPOPPE AWASHANGAA WANAOWAVAMIA VIONGOZI SIMBA

Picha
Na Juma JR, DAR ES SALAAM Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amewashangaa watu ambao wamekuwa wakijitokeza kuwavamia au kuwalaumu viongozi wa Simba ambao wanatoa kila kitu kadiri ya uwezo wao kuhakikisha timu inafanya vizuri. Kama hiyo haitoshi, Hans Poppe amesema, beki Hassan Kessy ambaye ameondoka Simba na kujiunga Yanga, waziwazi aliwasaliti. “Viongozi hawachezi pale uwanjani, kawaida wanafanya kila kitu kuhakikisha wachezaji wanapata na kwenda kucheza. “Wao ndiyo wanatakiwa kuwa na moyo na klabu, wawe na huruma na mashabiki. Lakini si mtu anapewa kadi nyekundu kwa makusudi kabisa, halafu ,mashabiki wanavamia viongozi. “Wakati mwingine nanyama kwa kuwa ukibishana na wajinga na wewe utaonekana ni mjinga. Lakini angalia alichokifanya Kessy, kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Toto ambayo inaonyesha huyu alipania kuipata. “Siku chache baadaye anajiunga na timu nyingine, tena kukiwa na tetesi nyingi kuhusiana na ushiriki wake nao. ...

YANGA SASA WAAMUA KUMFUATA NGASSA 'SAUZI'

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MABINGWA wa soka nchini Yanga SC wameachana na ziara yao ya nchini Uturuki na sasa wameamua kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi yao ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya makundi Robo fainali. Uongozi wa Yanga kupitia mwenyekiti wake wa Kamati ya mashindano Issack Chanji wamemua kubadili ratiba yao ya kuelekea Uturuki ambapo ni karibu kabisa na Algeria ambapo watakwenda kukabiliana na MO Bejala ya Algeria mchezo wa kwanza  kombe la Shirikisho. Yanga imetinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika hivyo italazimika kukutana na timu za MO Bejala ya Algeria, TP Mazembe ya DRC na Medeama ya Ghana. Kwa maana hiyo Yanga itakuwa imemfuata mshambuliaji wake wa zamani Mrisho Ngassa anayekipiga Free State Stars inayoshiriki Ligi kuu Afrika Kusini Yanga SC sasa wanakwenda Afrika Kusini

TAIFA STARS YAISHIKA HARAMBEE STARS

Picha
Na Salum Fikiri Jr, NAIROBI TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jioni ya leo imeilazimisha sare ya 1-1 timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars mchezo wa kirafiki wa kimataifa uwanja wa Moi Kasarani jijini Nairobi. Ikicheza kwa kujiamini, Taifa Stars ilikuwa ya kwanza kujipatia bao la uongozi lilikofungwa na mshambuliaji wake Elius Maguli aliyepokea krosi murua ya beki wa pembeni Juma Abdul Mnyamani. Harambee Stars iliyoonekana kususiwa na mashabiki wake ilijipatia bao la kusawazisha lililofungwa na mshambuliaji wake wa kimataifa anayekipiga Southmpton ya England Victor Wanyama na kuikoa nchi yake kulala mbele ya vijana wa Charles Boniface Mkwassa Taifa Stars

YANGA YAWAENDEA MO BEJALA UTURUKI

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM YANGA SC wataweka kambi yao bchini Uturuki katika maandalizi yao hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Mo Bejala ya Algeria. Mabingwa hao wa bara, Ngao ya Jamii na kombe la FA, wataondoka nchini mara baada ya kumalizika kwa likizo kwa wachezaji wake ya siku tano ambapo wachezaji wake wengine wamejiunga na timu za taifa. Haruna Niyonzima (Rwanda), Vincent Bossou (Togo), Deo Munishi, Mwinyi Hajji, Deus Kaseke na Juma Abdul (Tanzania), wachezaji hao wataungana na wenzao wengine kuanza safari ya Uturuki. Kamati ya mashindano ya Yanga Sc imeketi na kocha mkuu wa mabingwa hao Mholanzi Hans Van der Pluijm kuzungumzia kambi ndipo Mholanzi huyo alipoichagua Uturuki kama sehemu sahihi kwa kujiandaa na Waalgeria hao. Hii ni mara ya tatu kwa Yanga Sc kwenda nchini Uturuki kuweka kambi, Yanga imefuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika na itacheza na timu za TP Mazembe, Madeama na Mo Bejala

REAL MADRID YATWAA UBINGWA WA ULAYA

Picha
REAL MADRID mabingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kuwalaza Atletico Madrid fainali kupitia mikwaju ya penalti. Mkwaju wa ushindi umefungwa na Cristiano Ronaldo. Mechi ilimalizika 1-1 muda wa kawaida na wa ziada. Real Madrid wanaonolewa na mchezaji wao wa zamani Zinedine Zidane ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa Sergio Ramos, licha ya kuingia bao hilo, Real walionekana kuishambulia Atletico. Kocha wa Atletico Diego Simione alifanya mabadiliko ya kumwingiza Carlossa ambaye ndiye aliyefanikiwa kusawazisha bao hilo na kufanya matokeo yawe 1-1. Mchezo huo ulimalizika kwa sare na kuelekea kwa dakika za nyongeza ambapo hata hivyo hazikufangana, ndipo mikwaju ya penalti ilipoanza kupigwa na Real kushinda kwa mikwaju 5-3, Ronaldo ndiye aliyefinga bao la ushindi hasa baada ya kipa wake kuokoa penalti ya Atletico

YANGA YAWAFUNGA MIAKA MITATU BARTHEZ, YONDANI NA OSCAR JOSHUA, SIMBA MPOO

Picha
Na Saida Salum, DAR ES SALAAM MABINGWA wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Ngao ya Jamii na FA Cup, Yanga SC leo imewaongeza mikataba mipya nyota wake watatu Oscar Joshua, Ali Mustapha 'Barthez' na Kevin Yondani. Wachezaji hao kila mmoja wamesainishwa mkataba wa miaka mitatu kwa maana hiyo wataendelea kukipiga na Yanga hadi mwaka 2019, Barthez alikuwa akitajwa katika usajili wa Simba SC pamoja na kiungo Salum Telela. Yanga imeamua kuwapa mikataba mirefu nyota hao hasa kutokana na msaada wao mkubwa waliouonyesa msimu huu wakifanikisha mataji matatu makubwa yaliyo chini ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF. Vilevile wachezaji hao wameisaidia Yanga kufuzu kwa mara ya kwanza na kuandika historia kuwa klabu ya kwanza nchini na Afrika mashariki kwa ujumla kuingia hatua ya makundi konbe la Shirikisho barani Afrika Kevin Yondani aneongezewa nkataba wa miaka mitatu Yanga

STAA WETU: ABDUL 'NAJ' MACHELA, MTOTO WA MCHEZAJI WA SIMBA ANAYETAMANI KUCHEZA VPL

Picha
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM WAHENGA wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka, Mshambuliaji wa zamani wa Simba katika miaka ya 90 akisifika kwa kupiga mashuti makali langoni kwa wapinzani wao, Ali Machela ndiye ninayemwelezea. Lakini mpachika mabao huyo hatunaye duniani lakini ametuachia mtoto wake ambaye naye amefuata nyayo zake, Abdul 'Naj' Machela ndiye mtoto wa straika huyo wa zamani wa Simba SC. Naj kama mwenyewe anavyooenda kujiita, ni mmoja kati ya wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu, ingawa anajiona kama hana bahati ya kusajiliwa na vilabu vya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL). Mwenyewe anajiona kama ana mikosi ya kupata timu kubwa na ameiambia Mambo Uwanjani kwamba anaumia sana anapoona watoto wa mastaa wa zamani wa Simba au Yanga na timu nyingine kubwa wanasajiliwa na vilabu vya ligi kuu huku yeye akiendelea kusota mchangani. 'Kwakweli sijisikii vizuri wenzangu wanasajiliwa na vilabu kama Yanga, Simba Nk huku mimi nikiendelea kucheza mchangani', ana...

NDULUNO JUNIOR AIBUKA NA T:SHIRT ZA KIJANJA

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM MBUNIFU wa mavazi anayechipukia hapa nchini Ndulumo Junior ameibuka na mavazi ya kijanja yawafaayo vijana wa kileo ambayo ni T;Shirt za rangi mchanganyiko na tayari zimeingia sokoni. Akizungumza leo na Mambo Uwanjani, Ndulumo Junior amesema ameamua kuwa mbunifu wa mavazi na ujio wake na T:Shirt za kijanja utamfanya akubalike na jamii hasa vijana ambao wameonekana kuzikubali haraka pamba zake. T:Shirt hizo zenye mchanganyiko wa rangi zimeandikwa 'Usi4C Nikuamini' na zinapatikana madukani, 'Kwa sasa nimezisambaza sehemu mbalimbali ikiwemo kwenye saluni za kike na za kiume pia Stationary na kwingineko', alisema mbunifu huyo anayemiliki duka la nguo Kariakoo jijini Dar es Salaam Ndulumo Junior mbunifu mpya wa mavazi anayechipukia, tayari ameshaachia viwalo vya maana Moja ya T:Shirt za Ndulumo Junior, mjanja changamkia fulsa hiyo upendeze

MOURINHO ATUA MAN UNITED AMWAGA WINO KUKINOA KIKOSI

Picha
JOSE Mourinho amesaini kandarasi ya miaka miwili kujiunga na 'Mashetani Wekundu' wa Old Trafford Manchester United na kuondoa uvumi uliozagaa kwa muda mrefu juu ya kujiunga kwake na mashetani hao. Mourinho kocha mbwatukaji mwenye rekodi za kutisha sasa anakuwa meneja mpya wa Man U timu iliyopoteza heshima yake mara baada ya kuondoka kwa Alex Ferguson maarufu kama Fergie. Meneja huyo atakuwa na kazi ya kurejesha mataji kama yale ya primia na UEFA Champion League, Mourinho anarithi mikoba ya Lous Van Gaal aliyetimuliwa juma lililopita licha ya kuibebesha taji la FA Cup

MICHANO: P- FUNKY MAJANI, DHARAU ZIMEMPOTEZA KWENYE MUZIKI

Picha
Na Mkola Man, TANGA YAP......yap.....yap....leo Michano inamchana prodyuza P Funky Majani ambaye anamchango mkubwa sana katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini Tanzania mastaa wote unaowajua walitoka kwake, kiufupi uwezi kuuelezea muziki wa hapa bongo bila kumtaja. Jina lake halisi ni Poul Mathiyas Khalfan ni chotala, ila dharau na kujiamini ndio chanzo cha anguko lake lililosababisha samaki aliowabeba waoze kisha akashindwa kustahimili changamoto baada ya Media kumkwamisha kwa kumvalisha miwani meusi gizani ili asione. Miwani hiyo yenye kiza ilimfanya ashindwe kuona mbele pale alipobadilisha mfumo wa muziki na kuwapa nafasi maprodyuza wengine waliokuwa hawajulikani na kuwapa nafasi kubwa kama wanaweza pasipo kuweza ikawapa moyo na uzoefu kwakuwa P Funky alikuwa anadili na mastaa tu pasipo wasanii wachanga. Na watu walikuwa wanataka ladha mpya nadhani akujua muziki ni kama biashara uwezi kuwabagua wateja, huyu ananunua sigara mwingine sukari mwisho wa siku wote ni watej...

TFF YAPULIZA KIPYENGA UCHAGUZI YANGA

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM SHIRIKISHO la mpira wa miguu nchini TFF limeutangaza rasmi mchakato wa uchaguzi mkuu wa mabingwa wa bara, Ngao ya Jamii na FA Cup Yanga SC na fomu za kuwania uongozi zikianza kutolewa Mei 27 katika ofisi za Shirikisho hilo uwanja wa Karume Dar es Salaam. Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF Wakili Aloyce Komba amesema wanachama wa Yanga wataanza kuchukua fomu za juwa ia uongozi kuanzia Ijumaa Mei 27, Komba amedai taratibu za kulipia ada za uanachama ili kushiriki uchaguzi huo hilo litafanywa na Yanga wenyewe. Aidha mwenyekiti huyo amedai Yanga wametakiwa kufanya uchaguzi chini ya TFF baada ya kukaidi kufanya wenyewe kwa nuda wa miaka miwili hivyo viongozi wao hawapo kisheria, ameelezea hupatikanaji wa fomu za nafasi ya uenyekiti na makamu wake zitaoatikana kwa shilingi laki mbili na zile za nafasi za ujumbe ni laki moja tu

TFF YAMWANGUKIA CANNAVARO

Picha
Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM RAIS wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF Jamal Emily Malinzi amemtaka Nahodha na mlinzi wa mabingwa wa ligi kuu bara, Ngao ya Jamii na FA Cup Yanga Sc Nadir Ali Haroub 'Cannavaro' kukubali arejee kwenye timu ya taifa, Taifa Stars. Cannavaro amekataa kujiunga na kikosi hicho hasa baada ya mwalimu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwassa kumvua ubahodha kimafia, awali Cannavaro alikuwa nahodha wa Stars lakini kocha huyo akamvua kimafia na kumvika kitambaa cha unahodha mshambuliaji wa Genk Mbwana Samatta. Kitendo hicho kilionekana kumuudhi Cannavaro na siku chache ya baadaye akatangaza kujiuzuru kuichezea Stars, lakini Mkwassa ambaye pia alikuwa kocha msaidizi wa Yanga akamteua tena kwenye kikosi chake kinachojiandaa kucheza mechi ya kirafiki na Harambee Stars. Beki huyo wa kati mwenye mafanikio katika klabu yake ya Yanga amekataa kujiunga na Stars, jana katika mchezo wa fainali kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup Uwanja wa Ta...

KIIZA ALIA KUNYIMWA UFUNGAJI BORA

Picha
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM MSHAMBULIAJI wa Simba raia wa Uganda Hamisi Friday Kiiza amesikitishwa na kitendo cha Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF kumnyima tuzo ya ufungaji bora na kumpa Atupele Green Jackson wa Ndanda FC. Akizungumza a mtandao huu, Kiiza amesema yeye ndiye mfungaji bora wa kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup kwani amefunga jumla ya magoli matano. Lakini anashangaa jana Shirikisho hilo limemtangaza Atupele Green wa Ndanda kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo wakati si kweli, Kiiza amefunga magoli mawili dhidi ya Burkina Faso ya Morogoro Simba ikishinda mabao 3-0 pia alifunga tena mawili dhidi ya Singida United Simba ikishinda 5-0 na alifunga bao moja dhidi ya Coastal Union, Simba ikilala 2-1. Atupele Green amefunga magoli manne lakini akapewa zawadi ya ufungaji bora, pia Kiiza anailaumu klabu yake kwakushindwa kumpanga kwenye mechi za mwishoni za ligi kwani anaaminj angemvuka Amissi Tambwe aliyeibuka mfungaji bora Hamisi Kiiza amenyimw...

KISA YANGA, TFF YAICHOMOLEA CECAFA KUANDAA KAGAME DAR

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM SHIRIKISHO la mpira wa miguu nchini TFF limeikatalia Baraza la vyama Afrika mashariki CECAFA kuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la Kagame iliyopangwa kufanyika Dar es Salaam. Rais wa Shirikisho hilo Jamal Malinzi amesema TFF haiwezi kukubali Tanzania iwe mwenyeji wa michuano hiyo kwavile imebanwa na ratiba ya michuano ya kimataifa, Tanzania itakuwa mwenyeji wa michuano ya CAF ambapo klabu ya Yanga itakuwa ikishiriki. Yanga imeingia hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika hivyo haitaweza kushiriki michuano ya Kagame iliyopangwa kuanza Julai mwaka huu wakati Yanga itakuwa kwenye Shirikisho. Kwa maana hiyo Yanga haitashiriki Kagame kwakuwa itakuwa sambamba na kombe la Shirikisho, Malinzi amedai kama Yanga haishiriki Kagame haitakuwa na maana kwani Yanga ina mashabiki wengi wanaoingia uwanjani hivyo kuna uwezekano kutopatikana kwa mapato, TFF imelitaka CECAFA kutafuta nchi nyingine kuandaa fainali hizo

ANAYEKUMBUKWA: PATRICK MAFISANGO, INJINI YA SIMBA ILIYOZIMIKA GHAFLA

Picha
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM SIMBA SC inahaha kusaka kiungo mchezeshaji mwenye uwezo wa hali juu kama ilivyokuwa kwa Patrick Mutesa Mafisango (Sasa Marehemu. Marehemu Mafisango alikuwa na kiwango kizuri na aliwakosha wengi hasa mashabiki wa Simba Sc, jamaa alikuwa na uwezo wa kumiliki mpira na kutengeneza nafasi kwa wenzake. Pengo lake halitazibika kamwe kwani alifariki katika ajali mbaya ya gari iliyotokea Mei 17 mwaka 2012 maeneo ya Chang' ombe Dar es Salaam. Mchezaji huyo ndio kwanza alirejea na wenzake nchini wakitokea Sudan walikokwenda kushiriki mchezo wao wa kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya 16 bora na Al Shandy ambapo Simba iliondoshwa kwa mikwaju ya penalti 8-7. Mafisango ni kati ya wafungaji hodari na alikuwa akiibeba Simba pale ibapoyumba, uwepo wake ulitengeneza kombinesheni kali ya Felix Sunzu na Emmanuel Okwi ambayo ilikuwa haikamatiki. Alizaliwa Machi 9, 1980 huko DRC na alibahatika kuzichezea timu mbalimbali katika maisha yake ya soka, alichukua ur...

YANGA NA AZAM HAPATOSHI LEO TAIFA, NI FAINALI YA FA CUP

Picha
Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM KLABU bingwa Afrika mashariki na kati Azam FC jioni ya leo inawavaa mabingwa wa Tanzania bara na wawakilishi pekee wa mashindano ya kimataifa Yanga SC mchezo wa fainali kombe la Shirikisho maarufu FA Cup uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Miamba hiyo kila inapokutana hukamiana sana na mwisho humaliza dakika tisini kwa mwendo wa sare hatimaye kupigiana penalti, mara ya mwisho kukutana kwenye mchezo wa mashindano ya mtoano timu hizo zilifungana kwa zamu. Katika mchezo wa Robo fainali kombe la Kagame uliofanyika uwanja wa Taifa mwaka jana, Azam ilishinda kwa matuta baada ya sare ndani ya dakika tisini, pia Yanga ikalipiza kisasi katika mchezo wa Ngao ya Hisani kwa mikwaju ya penalti. Pambano la leo litakuwa gumu hasa kutokana na vikosi vya timu zote kuimarika, Yanga ikiwa na hamasa ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika pamoja na kutwaa ubingwa wa bara, Azam itataka kuwahakikishi mashabiki wake kwamba walistahili ubingwa wa Kagame, Ng...

YANGA YAPANGWA KUNDI MCHEKEA KOMBE LA SHIRIKISHO

Picha
YANGA SC ya Tanzania leo imepangwa kwenye makundi kombe la Shirikisho barani Afrika ikionekana imewekwa kwenye kundi jepesi ama mchekea kwa lugha nyingine. Shirikisho la mpira wa miguu brani Afrika CAF limeipanga Yanga ns timu za Mo Bejala, TP Mazembe na Medeana, kwa kundi hilo ni dhahili Yanga itakuwa na timu mchekea kwani hata TP Mazembe ya sasa si ile iliyopita. RATIBA YA KUNDI A || MECHI ZA YANGA - MO Bejaia vs Young Africans (17 June 2016) - Young Africans vs TP Mazembe (28 June 2016) - Young Africans vs Madeama (15 July 2016) - Madeama vs Young Africans (26 July 2016) - Young Africans vs MO Bejaia (12 August 2016) - TP Mazembe vs Young Africans (23 August 2016) Taarifa kutoka Website ya CAF - Afrika

TSHABALALA AWA MCHEZAJI BORA WA SIMBA APRILI

Picha
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM BEKI wa kushoto wa Simba Sc Mohamed Hussein 'Tshabalala' amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa klabu ya Simba wa mwezi Machi na Aprili mwaka huu imeelezwa. Kupitia mtandao wa Simba Sc Tanzania, Tshabalala amechaguliwa kuwa mchezaji bora baada ya kutoa msaada mkubwa ndani ya klabu hiyo iliyomaliza kwenye nafasi ya tatu ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara. Tshabalala ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars amekuwa katika kiwango kizuri siku za hivi karibuni na kuwashangaza watu mbalimbali wanaofuatilia mchezo huo

BABA MANYIKA AMKATIA TAMAA MWANAYE

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM BABA wa kipa wa Simba Sc Manyika Peter Manyika amemkatia tamaa mwanaye Peter Manyika kwa madai hawezi kurejea tena kwenye makali yake kwa sababu alishindwa kuzingatia maagizo yake. Akizungumza na Mambo Uwanjani hivi karibuni, Manyika amesema, mwanaye ameshindwa kuzingatia maagizo yake kwani alilewa penzi la Video Queen wa bongofleva. Manyika aliyewahi kuitwa Tanzania One amedai mwanaye huyo hawezi tena kuitwa Tanzania One kama alivyokuwa yeye hapo zamani kwavile hakuzingatia mafundisho yake, Manyika ameanzisha chuo chake cha kuwanoa makipa mbalimbali akiwemo mwanaye lakini anashangaa anashuka kiwango kila kukicha. Kipa huyo aliyewahi kutamba akiwa na Mtibwa Sugar, Sigara, Yanga Sc na Taifa Stars, amesikitishwa na kiwango cha mwanaye ambaye kwa sasa anatumika kama kipa wa akiba wakati hapo mwanzo aliaminika langoni akianza kama kipa chaguo la kwanza Peter Manyika wa Simba anadaiwa kushuka kiwango

BAKHRESSA AMPELEKA BURE FARID TENNERIFE

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MKURUGENZI wa timu ya Azam Fc ya Dar es Salaam Yussuf Said Salim Bakhressa aneamua kumpeleka bure winga wake Farid Mussa Marik hasa baada ya kufaulu majaribio yake katika timu ya Tennerife ya Hispania. Farid alikwenda kufanya majaribio kwenye timu hiyo inayoshiriki ligi Daraja la kwanza maarufu Sagunda Division na kufaulu lakini timu hiyo imeitangazia Azam dau dogo ikitaka kumnunua. Lakini bosi huyo ambaye pia ni Wakala wa kimataifa anayetambuliwa na Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA, Bakhressa ameona ni bora amruhusu kinda huyo kujiunga bure na Tennerife na baadaye akitakiwa na timu nyingine Azam itanufaika

LVG AFUNGASHIWA VIRAGO MAN UNITED

Picha
KLABU ya Manchester United ya England imetangaza kumfuta kazi meneja wake Lous Van Gaal (LVG) licha ya kufanikiwa kuibebesha taji la FA Cup mwishoni mwa juma lililopita. Van Gaal ameondoshwa kwenye kikosi hicho hasa baada ya kushindwa kuipa taji la primia na kujikuta ikiangukia nafasi ya tano, Man United imepoteza makali yake tangia alipoondoka Babu Alex Ferguson. Kocha huyo Mdachi alichukua mikoba ya Mskochi David Moyes ambaye naye alifurushwa hasa kufuatia kufanya vibaya kwa klabu hiyo kongwe, tayari Man United imethibitisha kutua kwa kocha mbwatukaji Jose Mourinho ambaye amewahi kuzinoa Porto, Chelsea, Inter Milan na Real Madrid

LVG AFUNGASHIWA VIRAGO MAN UNITED

Picha
KLABU ya Manchester United ya England imetangaza kumfuta kazi meneja wake Lous Van Gaal (LVG) licha ya kufanikiwa kuibebesha taji la FA Cup mwishoni mwa juma lililopita. Van Gaal ameondoshwa kwenye kikosi hicho hasa baada ya kushindwa kuipa taji la primia na kujikuta ikiangukia nafasi ya tano, Man United imepoteza makali yake tangia alipoondoka Babu Alex Ferguson. Kocha huyo Mdachi alichukua mikoba ya Mskochi David Moyes ambaye naye alifurushwa hasa kufuatia kufanya vibaya kwa klabu hiyo kongwe, tayari Man United imethibitisha kutua kwa kocha mbwatukaji Jose Mourinho ambaye amewahi kuzinoa Porto, Chelsea, Inter Milan na Real Madrid

MAONI: KAULI ZAKO HANSPOPPE ZINAWACHOSHA WANASIMBA

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM MWENYEKITI wa Kamati ya usajili wa klabu ya Simba Kapteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Zacharia Hanspoppe amekuwa na majibu ya kuudhi na kukera wapenzi na mashabiki wa Simba. Kuna wakati najiuliza kati ya yeye na wapenzi na mashabiki wa Simba nani hasa wenye uchungu pale timu ibapotokea imefanya vibaya, Hanspoppe anashindwa kuwa na kauli nzuri kwa Wanasimba hasa wapenzi wanapotaka kupewa matumaini. Hanspoppe chini ya kamati hiyo bdiyo imekuwa ikihusika kusajili na kuacha wachezaji, mwenyewe anadai ni mapendekezo ya kocha, lakini kimtazamo si kweli, Kocha anatoaje mapendekezo wakati hayupo. Simba itaingia msimu ujao bila kocha huyu wa sasa, kila msimu Simba imekuwa ikianza na mwalimu mpya, kuna mipango imeandaliwa ya kumtosa Jackson Mayanja na tayari mchakato wa kuajili kocha mpya umeshaanza. Muda wowote Simba itamtangaza kocha mpya na anatajwa Milovan Cirkovic raia wa Serbia, pia Bobby William raia wa Ubelgiji naye yumo kwenye rada ...

BARTHEZ AINUSURU YANGA KULALA MBELE YA MAJIMAJI

Picha
Na Exipedito Mataruma, SONGEA MABINGWA wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga Sc jioni ya leo imenusurika kichapo mbele ya Majimaji ya Songea Uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma baada ya kutoka sare ya 2-2 mchezo wa ligi kuu bara. Yanga imefikisha pointi 73 ambazo hazikuweza hata kusogelewa na timu yoyote, Yanga ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza lililofungwa na Poul Nonga, Majimaji walisawazisha kupitia Alex Kondo yote yamefungwa kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili Majimaji walilisakama lango la Yanga kama nyuki na kufanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na Said Mrisho, Yanga walisawazisha bao kwa njia ya penalti likifungwa na kipa wake Ali Mustafa 'Barthez', goli hilo limeinusuru Yanga kwani ingeweza kulala na kuharibu cv yake

SIMBA YAMBEBA KIBADENI, YADUNDWA 2-1 TAIFA

Picha
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM SIMBA SC jioni ya leo imeendeleza machungu kwa mashabiki wake hasa baada ya kuduwazwa mabao 2-1 na vijana wa Abdallah Kibadenj JKT Ruvu Uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo wa mwisho wa ligi kuu bara. Vijana wa JKT Ruvu ndio walioanza kulisakama lango la Simba lakini mabeki wa timu hiyo walikuwa makini, mabao ya JKT Ruvu yamewekwa kimiani na Abdul Omari yote akifunga kipindi cha kwanza. Simba waliamka kipindi cha pili wakipata bao la kufuatia machozi lililofungwa na nahodha wake Mussa Hassan Mgosi, KATIKA mchezo mwingine uliofanyika uwanja wa Azam Complex Chamazi, Azam imeifunga 1-0 Mgambo JKT na kuishusha daraja. Azam sasa amekamata nafasi ya pili ikiiacha nyuma Simba Sc iliyokamata nafasi ya tatu

JUMA ABDUL AWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI APRILI

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM BEKI wa kulia mwenye mambo adimu wa Yanga Sc Juma Abdul Jaffari Mnyamani leo ametangazwa na Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF kuwa mchezaji bora wa mwezi Aprili baada ya kuwashinda wenzake. Abdul sasa atajinyakulia kitita cha Vodacom shilingi Mil moja, beki huyo amekuwa bora hasa baada ya kuonyesha kiwango kikubwa ndani ya mwezi Aprili kuisaidia Yanga kutwaa ubingwa wa bara. Beki huyo aliyesajiliwa misimu miwili iliyopita akitokea Mtibwa Sugar ya Morigoro amekuwa katika kiwango kizuri na kumfanya kocha mkuu wa timu ya taifa Charles Boniface Mkwassa kumjumuhisha kwenye kikosi chake Juma Abdul Jaffar mchezaji bora Aprili mwaka huu

DANGOTE KUIMWAGIA MAPESA NDANDA FC

Picha
Na Saida Salum, MTWARA BILIONEA Aliko Dangote raia wa Nigeria anatajwa kuwekeza kwenye timu ya ligi kuu ya Ndanda Fc ya mjini hapa, endapo bilionea huyo namba moja barani Afrika atawekeza kwenye timu hiyo basi tutegemee mabadiliko makubwa. Habari ambazo bado hazijathibitishwa zinasema bilionea huyo mwenye viwanda vya kutengeneza Cement ya aina yake ya Dangote inayouzwa kwa gharama nafuu. Bilionea anatajwa kuichukua timu hiyo kama mdhamini hivyo kutawafanya Ndanda kuogelea manoti, hii ni mara ya pili kwa Ndanda kupata wafadhili kwani tayari ilishaonja noti za mfanyabiashara wa matairi Nassoro Binslum ambaye hata hivyo ameachana na Ndanda

SIMBA NA JKT RUVU NI KUSUKA AU KUNYOA, YANGA NA MAJIMAJI NGOMA INOGILE

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM LIGI kuu ya Vodacom Tanzania bara inafikia hatamu leo kwa vilabu vyote  vinavyoshiriki ligi hiyo, tayari mabingwa wa ligi hiyo wameshajulikana ni Yanga Sc na vita pekee imehamia kusaka mshindi wa pili na zitakazoshuka daraja. Ligi hiyo inaendelea leo lakini mechi zinazosubiriwa kwa hamu ni tatu ti zitakazoshirikisha vigogo vya soka hapa nchini, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Simba Sc wanaikaribisha JKT Ruvu wakati pale Chamazi Azam Fc wataialika JKT Mgambo ya Handeni Tanga. Pambano lingine kali litakuwa mjini Songea kati ya mabingwa wa ligi hiyo Yanga Sc na wenyeji Majimaji ya Songea, uhondo wa ligi hiyo upo kwenye nafasi ya pili kati ya Simba na Azam. Azam inashika nafasi ya pili na pointi 63 wakati Simba ina pointi 62 zote zikiwa zimecheza mechi 29 na leo itajulikana nani atashika nafasi ya pili, pia vita itakuwepo katika janga la kushuka daraja ambapo tayari timu ya Coastal Union imeshashuka daraja, vita hiyo sasa ipo kwa timu mbili zitazoungana ...

STAA WETU: DEOGRATUS MUNISHI 'DIDA', SHUJAA WA YANGA NA TANZANIA KWA UJUMLA

Picha
Na Exipedito Mataruma, DAR ES SALAAM MACHO yake yalikuwa makini kuitazana penalti iliyopigwa dakika ya 87 zikisalia dakika tatu mpira kumalizika, si mwingine ni Deogratus Boniventure Munishi maarufu kama Dida akifananishwa na kipa wa Brazil Nelson Dida. Dida alikuwa shujaa Jumatano iliyopita ikifanikiwa kuiondosha mashindanoni GD Sagrada Esperanca ya Angola kwa jumla ya mabao 2-1, Yanga ilishinda magoli 2-0 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam shukrani kwa Simon Msuva na Matheo Antony waliofunga mabao safi kabisa. Yanga ilifungwa bao 1-0 katika Uwanja wa Esparanca mjini Dundo Angola goli lililofungwa na mkongwe Love Caburunca, matokeo hayo yameivusha Yanga hadi hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika ikiwa ni historia katika ukanda wa Afrika mashariki. Yanga inakuwa timu ya kwanza ya nchini kufikia hatua hiyo, pia ikumbukwe Yanga iliwahi kufanya hivyo mwaka 1998 ilipotinga makundi ligi ya mabingwa barani Afrika. ALIFIKAJE YANGA! Dida alianza kuchomoza akiwa na Manyema ya Ilala a...

WABABE YANGA WATUA NA DEGE LA SOUTH AFRIKA, MASHABIKI WAFURIKA

Picha
Na Exipedito Mataruma, DAR ES SALAAM YANGA SC imewasili jioni ya leo wakitokea nchini Afrika Kusini ambako nako walitokea Angola walikofanikiwa kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika. Msafara wa wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa Yanga ulitua majira ya saa tisa alasiri na kulakiwa na maelfu ya mashabiki wa timu hiyo ambapo msafara huo ulielekea makao makuu ya klabu mtaa wa Jangwani na Twiga Dar es Salaam. Yanga ilifungwa bao 1-0 na GD Sagrada Esparanca katika mchezo wa marudiano uliofanyika Jumatano iliyopita uwanja wa Esparanca mjini Dundo nchini Angola, Yanga imeitoa Esparanca kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya kushinda 2-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Dar ea Salaam Ndege ya South Afrika iliyowabeba Yanga ikikaribia kutua Mashabiki wa Yanga waliojitokeza kuilaki timu yao Watu ni wengi sana wakiilaki Yanga Kikundi cha mashabiki wa Yanga wakishangilia Bango likisomeka hivi Furaha iliyoje kwa mashabiki wa Yanga leo

DIAMOND AZIDI KUPAA KIMATAIFA, ATAJWA TUZO ZA BET

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MSANII wa muziki wa kizazi kipya maarufu bongofleva Naseeb Abdul ama Diamond Platinumz ametajwa kuwania tuzo mashuhuri nchini Marekani za BET ambazo zinajumuhisha wanamuziki maarufu duniani kote. Diamond ametangazwa kuwa miongoni mwa wanamuziki mashuhuri ukanda wa Afrika mashariki kuwania tuzo hizo ikiwa ni mara ya pili tangia alipoteuliwa mwaka jana. Msanii huyo mwenye rekodi ya kutwaa tuzo mbalimbali amekuwa pekee katika ukanda huu kuwania tuzo hizo, Diamond sasa atakula sahani moja na mastaa mbalimbali duniani kama Rihhana, Drake, P-Diddy, 50 Cent na wengineo ambao ni wasanii wakubwa Diamond Platinumz ametajwa kwenye tuzo za BET

MICHANO: BELLE 9 NI KAMA MWANARIADHA MWENYE NGILIMAJI

Picha
Na Mkola Man, TANGA YAP.....yap.....yap...Michano leo inamchana Belle 9 Mruguru asiye na bahati ama asiye na mipango ya ushindi kila anaposhiriki kwenye tuzo uangukia pua. Ingawa anauwezo wa kushinda kabisa ila hushindwa japo nyimbo zake ni nzuri kuliko anaoshindana nao. Baadhi ya nyimbo zake ni kama vile 'Sumu ya penzi', 'Masogange'. 'Amerudi', 'Ladha' na nyinginezo, pia amekuwa daraja kwa wasanii waliopata mafanikio. Ninachoamini mimi bado ajajua maana ya mashindano ama anajiamini sana, dunia ya leo kila unachokiona kizuri ujuwe kimetangazwa kupitia vyombo vya habari, siyo Tv na redio peke yake kama anavyofanya yeye. Belle 9 ni kama mwanariadha anayekimbia akiwa na ngilimaji kiufupi hawezi kushinda, Michano inamshauri abadilike kwani mashabiki wake wanatamani ushindi wake. Tukutane Wiki ijayo kwenye Michano ya Mkola Man Mwanatanga

YANGA WATAMBA KUILIPIA SIMBA DENI LA MOSOTI FIFA

Picha
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM YANGA SC wametamba kuilipia Simba Sc deni lake inalodaiwa na mchezaji wake wa zamani Mkenya Donald Mosoti aliyeshinda kesi FIFA na kutakiwa alipwe shilingi Mil 64 ama sivyo FIFA wataishusha daraja timu hiyo kongwe. Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga Sc Jerry Muro amesema Yanga hawako tayari kuiona Simba ikishushwa daraja kwani soka la Tanzania litaporomoka. Akizungumza kwa hisia, Muro amedai hatanii ni ukweli kwamba watawalipia deni hilo kwani kuna uwezekano mkubwa Yanga ikakosa kushiriki hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika iwapo FIFA itaifungia Tanzania kutokana na kosa la Simba

MASHUJAA YANGA KUWASILI KESHO SAA 8 MCHANA, KUINGIA KAMBINI KUWAVAA MAJIMAJI

Picha
Na Exipedito Mataruma, DUNDO MASHUJAA wa Tanzania Yanga Sc walioweka historia jana ya kuwa timu ya kwanza nchini na ukanda mzima wa Afrika mashariki na kati kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuiondosha GD Sagrada Esparanca ya Angola kwa jumla ya mabao 2-1. Yanga jana ilifungwa bao 1-0 katika uwanja wa Esparanca mjini Dundo Angola, licha ya kipigo hicho Yanga imefuzu hatua ya makundi baada ya kutangulia kushinda mabao 2-0 yaliyofungwa na Simon Msuva na Matteo Antony. Mabingwa hao wa bara watawasili nchini kesho wakitokea nchini Afrika Kusini ambako nako wamewasili wakitokea Angola, Yanga watatua saa nane mchana lakini moja kwa moja wataingia kambini kujiandaa na mchezo wao wa ligi kuu bara dhidi ya Majimaji utakaopigwa mjini Songea Jumamosi

ALI KIBA AINGIA ANGA ZA CHRIS BROWN

Picha
MSANII wa muziki wa bongofleva Ali Kiba leo akiwa nchini Afrika Kusini amesaini mkataba mkubwa na kampuni ya SONY MUSIC ambayo pia inafanya kazi na wasanii wakubwa kama Chris Brown, Davido na John Legend. Kiba aliyeachia wimbo wake mpya 'Aje' aliondoka jana kuelekea 'Bondeni' kwa Jacob Zuma na leo ameweka historia mpya kwenye tasnia ya muziki Tanzania. Msanii huyo sasa atafanya kazi chini ya usimamizi wa kampuni hiyo kubwa ambayo imeshawasaidia wanamuziki mbalimbali duniani kutambulika Ali Kiba akiwa anashikana mikono na mmoja wa mabosi wa Sony Music leo nchini Afrika Kusini

NGASSA AITUMIA SALAMU ZA PONGEZI YANGA

Picha
MSHAMBULIAJI wa kimataifa raia wa Tanzanja anayekipiga Free State Stars inayoshiriki Ligj kuu ya ABSA ya nchini Afrika Kusini Mrisho Ngassa ameitumia salamu za pongezi Yanga Sc kwa kufanikiwa kuingia hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika. Akizungumza na Mambo Uwanjani kutoka Afrika Kusini, Ngassa aliyewahi kuzichezea Yanga Sc  Simba na Azam amedai hatua iliyofikia Yanga ni ya kupongezwa. Yanga jana ilifungwa bao 1-0 na GD Sagrada Esparanca ya Angola lakini ikafuzu kwenda kwenye hatua ya makundi hasa baada ya kushinda 2-0 mjini Dar es Salaam Yanga Sc wamefuzu hatua ya makundi Afrika

YANGA YATINGA ROBO FAINALI AFRIKA, DIDA AWA SHUJAA

Picha
Na Exipedito Mataruma, ANGOLA YANGA SC ya Tanzania jioni ya leo imefanikiwa kuingia Robo fainali ya kombe la Shirikisho baranj Afrika licha ya kulala 1-0 na wenyeji wao GD Sagrada Esparanca ya Angola mchezo uliokuwa na figisu nyingi uliofanyika Dundo Angola. Esparanca wakitumia vema uwanja wao wa nyumbani wakibebwa na mwamuzi wa mchezo ikishuhudiwa wachezaji watano wa Yanga wakionyeshwa kadi za njano na mwingine nyekundu. Beki na nahodha wa Yanga Nadir Haroub Cannavaro alipewa kadi nyekundu, kipa wa Yanga Deo Munishi 'Dida' alicheza vizuri na kuibuka shujaa, Yanga waliruhusu bao kipindi cha kwanza na ilionekana dhahili kama wangepoteza mchezo huo. Eaparanca walipewa penalti zikiwa dakika za lala salama lakini Dida akafanikiwa kupangua mpira huo, Kwa maana hiyo Yanga sasa imefuzu Robo fainali itakayochezwa kwa mtindo wa makundi, HONGERA YANGA SC

ANAYEKUMBUKWA: JUMA NASSORO PONDAMALI "MENSAH", ALIKUWA KIPA NWENYE VITUKO LANGONI

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM KATIKA historia ya magolikipa hapa nchini wapo wengi kama vile Peter Manyika (Senior), Chachala Muya, Kichochi Lemba, Abdul Kipyenga, Spear Mbwembwe, Issa Manofu na wengineo ambao walitaka kumuiga Juma Pondamali 'Mensah' kwa vituko na mbwembwe zake akiwa langoni, lakini hawakumfikia hata robo yake. Pondamali alikuwa ni wa aina ya kipekee ndani ya nchi hii ambaye kwa sasa ndiyo anawanoa makipa takribani wote wa mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga Sc inayonolewa na Mholanzi Hans Van der Pluijm na msaidizi wake Juma Mwambusi. Achana na yote, Pondamali anashikilia rekodi ya utukutu, kipa huyo alifungiwa mara tano, na pia mara nne mapambano yalivunjika, Pondamali alizaliwa mwaka 1957 jijini Dar es Salaam katika Hospitali ya Ocean Road. Pondamali alipata masomo yake akianzia shule ya msingi Mlimani na baadaye Karume kabla ya elimu yake ya sekondari kuipata Mzizima muda wote huo wa utoto wake soka likiwa ndani ya damu yake. KOCHA MZUNGU AMWIBUA JANGWAN...