KIPRE TCHETCHE ASAINI AL NAHDA YA OMAN, AZAM WAHAHA
Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Azam FC raia wa Ivory Coast amesaini mkataba wa kuichezea Al Nahida ya Oman na sasa ameachana rasmi na Azam.
Taarifa zilizoenea leo zinasema mshambulizi huyo pia anawindwa na mabingwa wa soka nchini Yanga SC, Tchetche ni mmoja kati ya washambuliaji bora kabisa waliokinukisha katika ligi kuu ya bara na ni miongoni mwa wachezaji walioipa ubingwa wa bara mwaka juzi.
Hata hivyo viongozi wa Azam wamekuja juu wakitaka suala la mchezaji kulifikisha FIFA kwani wanadai Tchetche bado ni mali na ana mkataba wa kuitumikia timu hiyo